Ni siku ngapi mtumishi/mwananchi akiandika barua ofisi inatakiwa imjibu?

Ni siku ngapi mtumishi/mwananchi akiandika barua ofisi inatakiwa imjibu?

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2016
Posts
2,633
Reaction score
2,297
Kichwa cha barua kinajieleza. Ni muda UPI mwananchi akipeleka malalamishi yake kimaandishi inatakiwa yajibiwe! Hapa reference iwe hizi local government.

Kama kipengele hicho kipo, naomba mniwekee quotation please.
 
Kwa utendaji wa ofisi nyingi za umma ni hadi ufuatilie majibu ya barua yako vinginevyo sahau. Hata hivyo, iliyokuwa Mamlaka ya Mji wa Kigamboni (KDA ) wao walikuwa wanajitahidi kujbu barua za wananchi.

Vv
 
Ndani ya siku saba unapaswa uwe umejibiwa kama bado unayohaki ya kwenda kuwauliza ofisini sababu ya kuchelewa huko. Kumbuka ni muhimu kuwa na dispatch wakati unamkabidhi muhusika barua aweze kusaini ili kuweka kumb.siku uliyomkabidhi,
 
Naweza kupata hiyo quotation kwa maandashi au ilipoandikwa?
 
Hawajajibu kitu. Sasa nini kinafuata? Muongozo tafadhali
 
siku 7.hata km hawajajibu hoja yako wakiri kupokea na watalishughulikia.
ila kuhusu utatuzi inategemea suala lako ni mtambuka au laa,la maamuzi ya mtu mmoja au bodi ikae,lahitaji upande mwingine ujitetee au ushauri wao.
 
Back
Top Bottom