Ni siku ngapi unahitaji kufanya kazi ili kununua iPhone 17 Pro yenye thamani ya dola 1,099 (TSh. 2,711,957)? Tazama katika nchi mbalimbali duniani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Bei ni moja, lakini upatikanaji unatofautiana sana, kipato ndicho kinachoamua.

Je, unajua ni muda gani watu wanapaswa kufanya kazi ili kununua iPhone 17 Pro yenye thamani ya dola 1,099 sawa na TSh. 2,711,957 katika nchi mbalimbali?

Nchini Uswisi, inachukua takribani siku 3 pekee, jambo linaloonyesha jinsi mishahara mikubwa inavyofanya simu ya bei ya juu kuwa rahisi kununuliwa kwa haraka.

Soma > Leo tarehe 9 September Apple wamezindua iPhone 17 series na accessories nyingine!

Lakini upande mwingine, nchini India inaweza kuchukua karibu siku 160, ili Mtu kununua Simu hiyo, inahitaji kuweka lengo la muda mrefu.

Unadhani kwa Tanzania itachukua Siku ngapi hadi Mtu kufikia bei hiyo ya Simu?

Tazama katika nchi mbalimbali duniani;
  1. Switzerland - Siku 3
  2. Marekani (USA) - Siku 4
  3. Canada - Siku 5
  4. Ufaransa - Siku 6
  5. Uingereza - Siku 7
  6. Singapore - Siku 8
  7. Poland - Siku 17
  8. Thailand - Siku 61
  9. Brazil - Siku 77
  10. Ufilipino - Siku 101
  11. India - Siku 160

​
 
Swala la kununua simu na nchi inahusiana nini?

Maana swala la kununua simu ni ishu binafsi kulongana na kipato cha mtu husika

Hata hapa Tanzania Kuna watu dakika moja tu hiyo hela washaipata
Nadhani hujalewa mada. Huu ni utafiti ambao umechukulia mambo yote yako constant, i.e hali halisi ya kipato cha nchi bila kujali utajiri, kipaumbele cha mtu etc...
 
Bongo itauzwa tsh ngapi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…