Kwani tatizo ni nini? Mradi msiwe wote vijana sana yaani labda wote mna miaka 20 hivi maana mtasumbuana. Ndoa ina mitihani mingi mnaweza nkawa mnagombana mara kwa mara kwa kuwa hamjajua jinsi ya kujibizana, kukiri makosa na kusameheana. Kila mmoja atataka kuwa mshindi kila mnapokorofishana. Vinginevyo umri kulingana si tatizo. Mimi nawajua mke na mme ambao wote walizaliwa 1974 lakini wanaishi vizuri. Pia tanbua kuwa kuna ndoa ambazo mke ni mkubwa kuliko mme lakini maisha yanaenda.