Ni suala la muda tu: CCM itabaki kuwa ya wanawake

Hujajibu swali, dunia kuwa ya zamani kwa hiyo maandiko pia ni ya zamani? Hivyo yasizingatiwe?
 
hio mbona kawaida wee huoni mashoga wanavojinadi huko mitandaoni na mitaani? na yanaelekea kukaribiana na idadi ya wanawake.

TZ na Africa sasa inaenda kuwa kama nchi za ulaya kwa kila jambo na ndo tunapoelekea.
Upo sahihi katika hili, kabisa. Ila kwa hapa TZ... Haya tusubiri!
 
Mama amejua kuzichanga karata vyema....

Hana maana kuwa amewatenga WANAUME...

Akina mama ndio wapiga kura....

Isisahaulike mh.Rais analenga "women empowerment"....na si kosa.....

SIEMPRE CHIFU MKUU HANGAYA aaamin [emoji120]
Wewe ni "ke" au "me"!!???
Huko CCM mmebarikiwa kushikiwa akili.
 
Awamu ya waimba taarabu na baikoko kazi mnayo tarajieni mipasho na maneno ya shombo kutoka malkia mtukufu Hangaya.
 
Hujajibu swali, dunia kuwa ya zamani kwa hiyo maandiko pia ni ya zamani? Hivyo yasizingatiwe?
maandiko yazingatiwe, ila pia tambua zama zimebadilika, usilinganishe miaka 1,000 ilopita na sasa hivi.

Kwa mfano: Enzi za kina musa binadam wapo waloishi mpaka kufikisha umri wa miaka 300 hadi 500. Hivi sasa ni nani mwenyeuwezo wa kufkisha umri wa miaka 300?

Afu vitabu vitakatifu havijakataza mwanamke kuongoza bali mwanaume atawale. Kuna uongozi na utawala.

Kiasilia mwanamume ameumbwa awe mtawala, kwa mwanamke
kuanzia maumbile, mabavu, misuli na nguvu tofauti na mwanamke alivofanyika kutoka kwa mwanamume.

Ila kwenye masuala mengine kama ya uongozi n.k ni jukumu la wote mwanamume na mwanamke, maana wote wamepewa ubongo na akili.
 
CCM hakitabakia kuwa cha Wanawake makini bali kitakuwa cha Wanawake wazee waliochubuka na mikorogo waroho wa Bia.
Usawa wa kijinsia isiwe kichaka cha kuweka watu wasio na uwezo kwenye uongozi, hakuna sababu yoyote inayohalalisha kuweka mtu asiye na uwezo kwenye uongozi
 
Leta evidence she is rejected material?? anyway na hii rejection kama ipo ina matter?? whether you like her not she is there to stay....tena ana haki ya kugombea kama mtanzania mwingine yeyote
Usawa wa kijinsia isiwe kichaka cha kuweka watu wasio na uwezo kwenye uongozi, hakuna sababu yoyote inayohalalisha kuweka mtu asiye na uwezo kwenye uongozi
 
Nini tofauti ya kuongoza na kutawala? Je, Rais JPM alikuwa anatawala au anaongoza? Hiyo moja, mbili ni hii[emoji116][emoji116]

Umesema zama zimebadilika, ni kweli si uongo. Kwa hiyo kama maandiko yaliagiza mwanamke asimtawale mwanaume, yanatakiwa kupuuzwa kwani yalilenga tu zama zile na si hizi?

Je, unajua kuwa maandiko yanasema yeyote anayepunguza au kuongeza maana ya maandiko ana hatia? Hii ni kusema kuwa yote yatapita, ila neno la MUNGU halitopita. Iko wazi mwanamke hajapewa mamlaka ya kumtawala mwanaume.

Huu si mfumo dume, bali ni agizo la yule aliyekuumba wewe na mimi.

Hivyo basi, maandiko hayabadiliki.
 
tatizo huelewi maana ya uongozi na utawala.

utawala maana yake ni nguvu asilia kutoka kwa Mungu. Ndo maana mfalme ni mtawala na anaamini ameteuliwa na Mungu.

Ila uongozi ni usimamizi anaokabidhiwa mtu na wanadam kwa msaada wa Mungu.

Mwanamke kuwa kiongozi bado haimuondolei mwanamume utawala. Maana hata kimaumbile mwanaume amewekewa nguvu na misuli zaidi ya mwanamke ili amtawale mwanamke na si mwanamke amtawale mwanamume.

Ila inapokuja swala la kuongaza, hilo ni jukumu na haki ya wote. Maana wote wamepewa akili. Usichanganye kutawala na kuongoza. Ni maneno mawili tofauti.
 
Ahsante, umesema utawala ni nguvu asilia kutoka kwa Mungu(kwa hiyo mwanaume atamtawala mwanamke), ni sahihi wala sipingi.

Pia umesema uongozi haukuwekwa na Mungu, uliwekwa na binadamu kwa msaada wa Mungu(bila uasilia).
Je, kuna tofauti gani kati ya kuwekwa na Mungu na kusaidiwa na Mungu?

Mbona tofauti uliyoweka haijakidhi haja yangu? Yaani kwa logic ya kawaida tu, hivi utawala(ambao ni nguvu asilia), uliwekwa vipi na Mungu?

Yaani uongozi si nguvu asilia ila utawala? Real? Kwa hiyo Saudi Arabia na baadhi ya mataifa ya kiarabu hayajui kutofautisha utawala na uongozi? Kwani yale hayaruhusu mwanamke kushika uongozi wa juu na kumuongoza mwanaume.

Kwa hiyo wameshindwa kutofautisha sio? Hebu make it clear kaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…