Katika maisha kuna mambo mengi yanachosha na kushangaza pia.yanaleta ukakasi.
_Mtu kakuamini anakueleza tatizo lake,kama hujui jinsi ya kumsaidia/kumshauri mwambie ukweli tu,usianze kumweleleza shida zako. Tatueni kero yake ikiisha muanzishe utatuzi wa kero yako.
_Uko ndani ya usafiri wa umma,kuna wasafiri wa kila aina wenye matatizo/mafikra kibao unazungumza ujinga mwanzo mwisho.Tulia kidogo acha watu wawaze wanayowaza.
_Umeenda kwenye msiba/harusi au kusanyiko lolote lile unawasiliana kwa simu kwa msauti mkuuuubwa!watu wote wanakata shingo kukushangaa wewe wala hujishtukii.
_Umeenda ofisi ya umma badala ya kueleza shida iliyokupeleka hapo,unalaumu mtoa huduma uliyekutana naye hapo juzi!Mimi nikusaidieje sasa!
_Umbea na usengenyi ni pacha wa mtu mweusi,haukwepeki!jaribu basi kutosengenya hadharani ya nini kujiongezea maadui?
_Jirani kajitutumua kanunua kigari chake,kama hutaki kumpongeza si ufanye tu kama hujaona!siyo unaanza kwanza gari yenyewe ya mkopo halafu mbayaaa!wewe unayo.
_Umenunua homthieta nyumbani kwako,unagonga mziki kama ukumbini...fungulia kwa mahitaji yako bhana.!
_Mama yako anahali mbaya hapo kwenu kisiju tu,nyumba inavuja,hata soler hana ni mzee na ni mgonjwa,lakini hapo kwako Kinondoni unafanya sherehe na marafiki kila wiki!!!!!
Ni tabia mbaya!