Ni Tanzania pekee ambapo pikipiki zinachukuliwa ni ajira rasmi kwa vijana

Ni Tanzania pekee ambapo pikipiki zinachukuliwa ni ajira rasmi kwa vijana

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Nilikuwa nafuatilia swala la ajira za Vijana katika mataifa mengine hasa yenye Population kubwa sana kama India na nimegundua kwamba India pamoja na kuzalisha pikipiki hizi za Boxer na kuwa na idadi kubwa ya tatizo la ajira ila hakuna mahali kokote kule Serikali ya India inajinasibu kwamba pikipiki ni ajira kwa vijana wa India na Serikali ya India haijawahi hamasisha vijana wao wajiajiri kwa kuendesha zile Boxer. Kwa kifupi Pikipiki Bodaboda sio ajira kule India na haiko kwenye rrecord za Serikali ya Undia.

Nikapitia pitia Nepali pia nchi masikini sana wana pikipiki nyingi sana pia ila kwenye Data za Serikali pikipiki sio sehemu ya ajira kwa vijana, kote Philipine huko.

Njoo sasa Bongo ambapo wajinga, huku Pikipiki ni ajira kamili kabisa na Serikali inatembea kifua mbele kwamba imetoa ajira kupitia pikipiki kwa Masikini wajinga.

Ila kwa watawala wao watoto wana wanapata akira kwa vimemo.

Pia usisahau ni Tanzania pekee ambayo Serikali yake inahamaisisha biashara za uchuuzi Barabarani, hata mataifa masikini Duniani bado hayahamaishi raia wake kufanya uchuuzu make wanajua uchuuzi hauna tija kwa nchi.
 
Ajira ni chochote chenye kuleta UJIRA....wa pesa ,mali ama chakula!!!

Kazi ya bodaboda nayo iko humo kundini....

Ajira ni ubunifu...hivi ubunifu ni jambo la kukariri?!!

Mtaani kwetu kuna Halfan Jebe Gongagonga veterani wa kukaba kwa bisibisi sasa hivi ni bodaboda....

Zambe Mgobo...kibaka maarufu wa kuvunja majumba ya watu...leo ni bodaboda.....

Ni wengi mno...wengi sana...

#Bodaboda ni ajira kwetu vijana
 
Back
Top Bottom