Vitambulisho walivyopewa hivi karibuni hao viongozi uliowataja ni vitambulisho vinavyoonyesha uraia wa mtu.
vile vya zanzibar ni vitambulisho wa ukazi sio vyo uraia .kumbuka Tanzania ni nchi moja na tuna uraia mmoja tu "watanzania" na hakuna nchi inayoitwa zanzibar hivyo basi zanzibar kwa kua sio nchi haiwezi ku issue ID ya uraia wa zanzibar coz hakuna uraia wa zanzibar ila kuna ukazi wa zanzibar kama makazi mengine ya kawaida tu.
kwa kusema hayo niseme tu kwamba Hakuna vitambulisho vya uraia viwili hapo.kitambulisho kinachokutambulisha kwamba wewe ni mkazi wa dsm huwezi kukifananisha na kile kinachokutambulisha kwamba wewe ni raia wa Tz. nadhan mmenielewa wadau[/QUOTE
----------------------- --------------------------- --------------------------
kwanza nakupongeza kwa kiswahili chako kizuri, mtiririko wa maelezo yako ni mzuri.
Kama Zanzibar wamepewa vitambulisho vya ukazi ina maana wakazi wa Tanga,Mtwara, Mbeya nk nao watapewa vitambulisho vyao?
Pili, kama ni vitambulisho vya ukazi ina maana hata wasio raia wa Tanzania(Bara na visiwani) watakuwa na haki ya kupata hivyo vitambulisho kisheria maana wanaishi katika hayo maeneo ndani ya Tanzania au?
Tatu, ina maana mtu atakuwa na kitambulisho cha uraia pia na kuwa na passport? Nilidhani passport ndo kitambulisho cha uraia wa mtu kwa nchi fulani. kwa bahati mbaya au nzuri nimeishi ktk nchi mbili tu (Tanzania na Marekani) sijui kama kuna nchi inayotoa vitambulisho vya uraia na kuwa na passport (kwa kusafiria nje ya mipaka) Mfano hapa Marekani mtu anatakiwa kuwa na kitambulisho kinachoonyesha ukazi wa jimbo analoishi na ni kwa yeyote haijalishi ni raia au mhamiaji je JMT wataruhusu hilo? (hii inaambatana na swali la pili)