Ni Tanzania pekee ambayo raia wake watakuwa na IDs mbili

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
31,248
Reaction score
13,244
Majuzi nilishangaa kuona wenzetu wa visiwani wakipewa vitambulisho vipya vya uraia wakiwamo rais wa huko Dr. Shein, ili hali wanavyo tayari vya kwao-Kitambulisho cha mkazi Z'bar.Nilitegemea kuwa vile vya kwao vitafutiliwa mbali ili wawe na kimoja tu.Hii inachekesha, na muungano huu kweli ni kiini macho tu.
 
Hujaeleweka sema Tanzania Visiwani
 
sio tanzania visiwani sema ZANZIBAR hata ukurewe na mfia pia visiwa na wao wana id mbili

Tanganyika ilikufa ikazaliwa Tanzania Bara,na huwa tunasherehekea sikukuu ya Uhuru wa Tanzania Bara 9 Dec siyo Tanganyika.Zanzibar ipo na wao hawataki kuiita Tanzania Visiwani.
 

Vitambulisho walivyopewa hivi karibuni hao viongozi uliowataja ni vitambulisho vinavyoonyesha uraia wa mtu.

vile vya zanzibar ni vitambulisho wa ukazi sio vyo uraia .kumbuka Tanzania ni nchi moja na tuna uraia mmoja tu "watanzania" na hakuna nchi inayoitwa zanzibar hivyo basi zanzibar kwa kua sio nchi haiwezi ku issue ID ya uraia wa zanzibar coz hakuna uraia wa zanzibar ila kuna ukazi wa zanzibar kama makazi mengine ya kawaida tu.

kwa kusema hayo niseme tu kwamba Hakuna vitambulisho vya uraia viwili hapo.kitambulisho kinachokutambulisha kwamba wewe ni mkazi wa dsm huwezi kukifananisha na kile kinachokutambulisha kwamba wewe ni raia wa Tz. nadhan mmenielewa wadau
 
Yaweza kuwa kweli kidogo.
 
 
 
Pia ni tanzania pekee yenye noti mbili tofauti za pesa na ziko kwenye mzunguko mmoja wa fedha.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Sio vitambulisho viwili tu ni Tanzania pekee ndiyo nchi inayoongozwa na marais wawili, bendera mbili, nyimbo za taifa mbili, mabunge mawili(Baraza la wawkilishi na bunge la muungano) maamiri jeshi wawili na watu wenye uraia wa nchi mbili ndani ya nchi moja!
 

Ndio maana itifaki pale U/Taifa huwa inawasumbua.
 
Pia ni tanzania pekee yenye noti mbili tofauti za pesa na ziko kwenye mzunguko mmoja wa fedha.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Aibu kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…