Ni Tanzania tu Rais wa Nchi anaitwa mpendwa naye kuchekelea!

Ni Tanzania tu Rais wa Nchi anaitwa mpendwa naye kuchekelea!

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
Wapigadili, walafi, mafisadi na matapeli wana akili sana. Kila kiongozi anayeingia madarakani humkalia kikao na kujua wapi anawashwa ili wamkune hapo hapo!

Hakuna Rais aliyewahi kuwa na mapenzi na watu wake Kwa hapa Tanzania kama Julius Nyerere lakini hatukuwahi kusikia akiitwa "Rais wetu mpendwa". Mwinyi hakuitwa "Rais wetu mpendwa". Mkapa ndiye kabisaa hakuhitaji sifa hiyo. Hata Jakaya na ubishoo wake hakuitwa Rais wetu mpendwa.

Kwa mara ya kwanza tumesikia Amiri Jeshi akiitwa mpendwa ni Awamu ya 5 ya Magufuli (mwendakuzimu) na muasisi wa sifa hiyo ni Paulo Makonda then Mawaziri wakafuata.

Awamu ya 6 kauli hii imepamba moto lakini inatolewa na wateule wa Rais tu na si vinginevyo. Hata Marekani, Rashia, Kenya, Uingereza, Brazili, Equador nk hatujawahi kusikia Mkuu wa Nchi akiitwa "Our Beloved President", aibu.

Kauli hii ina Siri kubwa ya utapeli wa kisiasa. Ni lugha ya ulaghai, wizi, woga, hofu na kujiweka karibu na Mamlaka kuficha upigani uliojificha. Hii ni lugha ya Sanaa ya mahusiano yadiyo na afya. Imagine Majaliwa anamwita SSH mpendwa, Tulia Ackson anamwita mpendwa, CDF na IGP nao wamwite mpendwa, hivi wajukuu zake, wanaye, mumewe wamwiteje?

Rais ogopa na ukatae kuitwa Rais mpendwa. Behind the phrase kuna kuna ajenda ya kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa usione maovu Yao. Kataa tena hadharani kama Nyerere alivyokataa kuitwa mheshimiwa akataka aitwe Ndugu. Ni kwa vipi unaweza kumwajibisha anayekuitwa mpendwa?

Lakini kama na wewe unafurahi kuitwa mpendwa basi tumejua wapigadili wamefanikiwa 100% maana tunaambiwa Kwa Sasa Kuna mashindano baina na kati ya wateule wako nani akaunti yake inasoma B's na mzembe gani akaunti yake inasoma Ms. Wawili miongoni mwao wameshagonga Ts. Hallelujah!
 
J Nyerere, ni Baba wa Taifa, ni kama mkulima anapoingia porini kutafuta eneo ,hukuya eneo ni vichaka na miti ya mimba...... Huyu Atabaki kua Bora.

Mkapa, akajitahidi masuanla TRA, Takukuru ,angalau akaacha Alama .

Rais Bora na atakayebaki kua Bora, ambaye Atabaki kuliliwa na wakukima, bodaboda, Wananchi wakila aina na Atabaki kuchukiwa na wauza madawa ya kulevya, mafisadi ,Upinzani uchwara unaojali tumbo

Sio mwingine ni Hayati JPM
 
Mkuu umenifanya nicheke sn, matapeli huwa yana njia nyingi sn, yanasoma udhaifu wa kiongozi haraka sn
 
Ingawa Mwalimu Nyerere ashawahi kuitwa Mheshimiwa sana Julius Nyerere
Tembelea majengo ya zamani ya wajerumani utakuta huko mawe ya uzinduzi yakiandikwa ivo
 
mheshimiwa akataka aitwe Ndugu. Ni kwa vipi unaweza kumwajibisha anayekuitwa mpendwa?
Muasisi nayeye alipigwa chini kwenye ubunge mpaka leo hana mamlaka tena, kuna yule mzee lugola alikuwa hadi anamkatia mauno ila akachanwa live na uwaziri ukafia kulee.

Hayo ni mawazo ya kufikirika tu.
 
Muasisi nayeye alipigwa chini kwenye ubunge mpaka leo hana mamlaka tena, kuna yule mzee lugola alikuwa hadi anamkatia mauno ila akachanwa live na uwaziri ukafia kulee.

Hayo ni mawazo ya kufikirika tu.
Lugola alikula hela za Lugumi bila kumgawia mwendakuzimu
 
Mpendwa akihimiza nchi itafunwe👇🐒🐒🐒
 
Back
Top Bottom