Sine r Winters
Senior Member
- Jul 10, 2012
- 110
- 15
Vp wakuu, ni taratibu zipi zinafatwa mpaka uweze kusajili kampuni? Na huwa zinasajiliwa taasisi gani?
NB: kampuni ya IT.
NB: kampuni ya IT.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ingia hapa wewe, halafu ukifaidika unaweza kunilipa hata hela ya soda...... Vince ForumVp wakuu, ni taratibu zipi zinafatwa mpaka uweze kusajili kampuni? Na huwa zinasajiliwa taasisi gani?
NB: kampuni ya IT.
Mkuu nakupa heshima zako.Mimi naweza kukusaidia kwenye mchakato mzima kuanzia name search,memorandum and articles of association mpaka pale utapewa certificate of Incorporation na BRELA.We niPM au nipigie simu namba 0769210807 tushauriane.Nimefungua kampuni kadhaa zikiwepo za IT na Telecoms kwa hivyo taratibu nazielewa sanaVp wakuu, ni taratibu zipi zinafatwa mpaka uweze kusajili kampuni? Na huwa zinasajiliwa taasisi gani?
NB: kampuni ya IT.
BRELA ndie wakala wa kusajili kampuni Tanzania. unapaswa kuchagua jina la kampuni kwanza. wao ukiwapa pendekezo la jina, wataangalia kama hakuna kampuni inayotumia, na kama hakuna watakuruhusu utumie. utapaswa kuandaa nyaraka mbili ambazo ni memorandum of understanding na article of association. hizi nyaraka zinapigwa mhuri na mwanasheria au mhasibu. sheria zetu zinahitaji wamiliki wa kampuni wawe kuanzia 2 na kuendelea. kuna gharama unazolipa moja kwa moja BRELA ambazo ni ada ya usajili na gharama ya kuangalia jina. kama ukishirikisha wataalam kama sisi, tutakuchaji gharama ya ku facilitate mchakato mzima. cha kufahamu, kampuni ni kama binadamu tu, kwa hiyo ikihitaji kufanya biashara inapaswa kwenda kwenye mamlaka husika kupata kibali cha kuendesha biashara. nilikuwa naweka msisitizo hapa, kampuni sio kibali cha kufanya biashara