BRELA ndie wakala wa kusajili kampuni Tanzania. unapaswa kuchagua jina la kampuni kwanza. wao ukiwapa pendekezo la jina, wataangalia kama hakuna kampuni inayotumia, na kama hakuna watakuruhusu utumie. utapaswa kuandaa nyaraka mbili ambazo ni memorandum of understanding na article of association. hizi nyaraka zinapigwa mhuri na mwanasheria au mhasibu. sheria zetu zinahitaji wamiliki wa kampuni wawe kuanzia 2 na kuendelea. kuna gharama unazolipa moja kwa moja BRELA ambazo ni ada ya usajili na gharama ya kuangalia jina. kama ukishirikisha wataalam kama sisi, tutakuchaji gharama ya ku facilitate mchakato mzima. cha kufahamu, kampuni ni kama binadamu tu, kwa hiyo ikihitaji kufanya biashara inapaswa kwenda kwenye mamlaka husika kupata kibali cha kuendesha biashara. nilikuwa naweka msisitizo hapa, kampuni sio kibali cha kufanya biashara