Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 15,335
- 29,114
Waswahili walisema “mjinga wakati wa kwenda”
Basi bhana, kipindi hicho ndo naingia mjini kutokea uswekeni kwetu ndani ndani huko. Nikafikia kwa jamaa wa kijijini kwetu 'aliyetusua' kiaina ikiwa ni safari yangu kuelekea masomoni, alikuwa na getho fulani hivi kali mnaita 'self container' likisheheni vitu vingi 'mashikoro mageni' kwangu.
Picha linaanza asubuhi jamaa anaamka kwenda kwenye pilika zake, hivyo nabaki mwenyewe. Alijitahidi kunielekeza namna ya kutumia baadhi ya vitu ikiwemo kupika na 'kuwasha' na kuzima video.
Japo niliitikia maelekezo lakini sikuambulia chochote hivyo ilinipasa kushinda njaa kila siku, huku nikijibu nimeshiba na vyombo nimeosha.
Ukweli ni kwamba nilikuwa nashindia matunda tu kwenye friji na bites kadhaa ambazo alipenda kuja nazo jioni, labda na upolo wa ubwabwa ikitokea amepika usiku na kubakia.
Kosa kubwa alilofanya, katika maelekezo yake hakuelekeza matumizi ya choo cha ndani, kipo chumbani hivyo aliamini najua cha kufanya.
Ni hivi vyoo vyenu vya kukaa, mfuniko uko saaafii intact kabisa kila nikiingia sioni 'tundu' la kulenga li wapi
Pona pona yangu ni choo cha nje ambacho ni kichafu sana kwa maana ni kama hakina matumizi, nimekuja kustukia ni kama siku mbili tatu zimepita... nikajicheka sana japo nilijipongeza kwa vile 'jamaa' hakunigundua.
Tukio lingine, mgeni wangu sasa nami nishakuwa wa 'mujini'.
Nimechemsha chai nikajaza kwenye ‘chupa' tayari kwa matumizi, kumbe bwana kanicheki ninavyochuja chai huku akichukua 'shule'.
Ile tupo mezani sijui nimejisahau kitu gani, kutupa jicho namwona mgeni wangu anachuja tena chai yake wakati wa kumimina! [emoji3]
Nisiwachoshe, nitarudi na ile ya kufungua friji na na kuiacha wazi ili kufurahia ubaridi![emoji23]
Mjinga wakati wa kwenda.