*****"NI #TUNDU_LISSU"*****

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Hapo zamani za kale rais Barack Obama wa Marekani aliwahi kumtembelea rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete katika hospital aliyofikia wakati amekwenda kutibiwa USA ili kumjulia hali. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kumuuliza maswali kadhaa rais Obama kwamba anawezaje kuongoza nchi kubwa na complicated kama Marekani? Obama alisema; Ni rahisi sana; Ni kuwa na cabinet ya watu yenye akili (intelligent cabinet)

Kikwete akamuuliza tena Obama; Utajuaje mtu unayemchagua kama ana akili? Obama akamjibu; Very Simple! - Yani rahisi sana. Obama Akampigia simu Hilal Clinton ambaye hakuwa ameambatana naye hospitalini hapo. Obama akaweka loud speaker.

Akamwambia; Hilal hebu nijibie swali hili ninalokwenda kukuuliza, baba yako na mama yako wana mtoto, ila huyo mtoto sio mdogo wako, sio dada yako na wala sio kaka yako. Je huyo mtoto ni nani?. Hilal akajibu; Very simple! Its me! (Rahisi sana, ni Mimi ) Obama akamuuliza Kikwete; Je umesikia ni nani!? Kikwete akajibu; Ndio nimesikia, ni Hilal. Basi wakaendelea na story zingine zikiwemo za Gesi, IPTL nk. Baada ya muda wa dk 15 Obama akaaga kuondoka.

Basi, baada tu ya Obama kuondoka, Kikwete akanyanyua simu yake na kumpigia simu waziri mkuu wake Mizengo Pinda; Pinda akapokea simu wakapeana salamu kwa wingi. Baada ya salaam, rais akamwambia; Pinda naomba unisikilize kwa makini na unijibu swali hili ninalotaka kukuuliza!. Pinda akajibu, ondoa shaka mheshimiwa. Mh. akamuuliza Pinda; Kwa mfano; baba na mama yako wana mtoto, ila huyo mtoto sio mdogo wako, sio kaka yako na wala sio dada yako! Je huyo mtoto ni nani? Mizengo Pinda akafikiria kama sekunde 30 hivi bila kujibu.

Mwisho wa siku akasema dah! Mh. Naomba unipe muda nifikilie nikipata jibu ntakuambia. Akakata simu. Pinda alikuwa amekaa karibu na Membe, Sitta, Lukuvi, Werema. Prof. Muhongo pamoja na Ana tibaijuka. Basi Pinda akajaribu kuomba msaada kwao ili wamsaidie kijibu swali hilo, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kumpa jibu kwa swali lile. Basi ilipofika jioni waheshimiwa kumbe wana gym yao (sehemu ya kufanya mazoezi) pale dodoma huwa wanapasha moto misuli.

Basi pinda kwa mbali akamuona Tundu Lissu akipasha! Akaamua kumfuata kwa karibu ili apate kumuuliza lile swali. Akamwambia; Mh. Lissu samahani bwana, naomba nikuulize swali! Lissu akasema, hakuna shida karibu; Pinda akasema, Eti kwa mfano, baba na mama yako wana mtoto ila huyo mtoto sio mdogo wako, sio kaka yako na wala sio dada yako. Je, huyo mtoto ni nani? Lissu kwanza akacheka, kisha akusema PM bwana! Huyo mtoto ni mimi![emoji23] Pinda akasema, aah! Unasema kweli!? [emoji86] Lissu akasema, Kweli mheshimiwa mtoto huyo ni Mimi!

Basi Pinda akamshukuru, kisha kwa haraka akaenda pembeni kidogo, akanyanyua simu yake na kumpigia Mh. Rais. Pinda akasema; hallo Mh. Nimepata jibu la swali lako. Rais kikwete akasema, eehe hebu niambie! Pinda akajibu. Mtoto huyo ni #Tundu_Lissu! Rais akamwambia; aah wapi umekosea! Huyo mtoto ni Hilal clinton![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
___________________________
Makala kwa hisani ya Chadema ndani ya Damu! #ChademaInBlood!!

Ni #SamuNgwegwe!! Siku njema! [emoji124][emoji124]
 
Post ya siku nyingi, imenikumbusha mbali sana
 
Duh ! , mamaee halafu tunategemea maendeleo na vision za watu vilaza kama hao , too sad . Taifa la viongozi vilaza
 

Shida hapa mimi naona ni kukariri bila kufahamu/kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…