Ni ubongo uliojaa makamasi tu ndiyo unaweza kuamini kuwa Marumo Galants FC ni Bora kuliko Yanga SC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
"Mfa maji aishi kutapatapa" hayo ni maneno machache yenye maana kubwa sana.

Nimewatazama vizuri sana marumo Fc, kwa kweli Wana mpira wakawaida tu Tena mpira unaochezwa na Yanga ni Bora zaidi kuliko wao Marumo.

Marumo Wanapambwa na wachambuzi wasiojua mpira na kufanya waonekane wao ni Bora sana kuliko Yanga.

Gemu ya Marumo waliyocheza na Mamelod walipoteza kwa Goli mbili kwa sifuri, Tena mamelod hawakuchezesha wachezaji wao waandamizi ndani ya timu na huo ndio umekua mchezo wa mamelod kupumnzisha wachezaji.

Marumo fc, wameshashuka daraja kilichobaki ni kukamilisha ratiba tu katika ligi yao huko ya south Africa.
Laiti Kama marumo wangewafunga mamelod ingekuwa ni habari kubwa sana, na hiyo ingetumika na kila mchambuzi wa Tanzania kuwatisha yanga.

Yanga Ina nafasi kubwa sana ya kushinda na kufika fainali kutokana na kikosi kilichopo chenye ubora.

Wachambuzi wasiojua mpira (hawana statistics) sijui huwa wanapata wapi nguvu ya kusifia timu utasema ni Barcelona au Real Madrid.

Endeleeni kusifia timu na kuacha kutazama au kuukubali ubora wa Yanga kwa kuwa tu, timu yenu pendwa imepigwa na imetolewa kwenye michuano ya kimataifa.

YANGA IS UNSTOPPABLE NA ITACHUKUA KOMBE LA CAF CONFIDERATION
 
Ubora wao unal8ngana kwa takwimu za kombe la shirikisho,hilo halipingiki
 
Nimewatazama vizuri sana marumo Fc, kwa kweli Wana mpira wakawaida tu Tena mpira unaochezwa na Yanga ni Bora zaidi kuliko wao Marumo. Marumo Wanapambwa na wachambuzi wasiojua mpira na kufanya waonekane wao ni Bora sana kuliko Yanga.
Tukuamini wewe au kocha Profesa Nabi? maana Nabi amesema kwa kuwa Marumo ni wazuri, anaingia uwanjani kuzuia Yanga isifungwe, na si kushambulia
 
WANANCHIIIIIII LEO NI SIKU AMBAYO TUNAENDA KUUONESHA ULIMWENGU KWAMBA YANGA INA UKUBWA KIASI GANI.MAKOLO
WAMEJARIBU KUIKUZA MARUMO KWA KILA NAMNA ILA LEO TUTAENDA KUWAONESHA YANGA NI NANI.
EWE MWANANCHI TEMBEA KIFUA MBELE KWANI LEO NDIO TUNAENDA KUINGIA FAINALI RASMI.
LEO MADUNDUKA YATALILIA CHOONI.
 
Tukuamini wewe au kocha Profesa Nabi? maana Nabi amesema kwa kuwa Marumo ni wazuri, anaingia uwanjani kuzuia Yanga isifungwe, na si kushambulia
Hakuna kocha anayesema kuwa wapinzani wake ni wepesi huyo ni mbumbumbu tu lakini kocha mwenye profession yake hawezi kusema wapinzani wake ni dhaifu zunguka duniani kote.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hawatoamini macho yao [emoji23]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…