Iwezekana una tatizo linalojulikana kitaalamu kama Hemorrhoids au piles. Hili ni tatizo la kuvimba kwa mishipa ya damu katika haja kubwa, aidha kwa ndani (internal hormorrhoids) au kwa nje (external homorrhoids). Tatizo hili huwapata watu wengi duniani, mfano data zinaonyesha kuwa kadri ya watu mil. 10 waishio marekani wana hemorrhoids. sababu ni nyingi, ila kubwa ni pressure kwenye mishipa ya damu kwenye haja kubwa inayosababishwa na constipation (kutumia nguvu unapojisaidia), ujauzito, kuharisha, umri (wazee), kufanya mapenzi kinyume na maumbile, nk.
dalili ni pamoja na kuwashwa, maumivu sehem za haja kubwa na wakati mwingine kuonekana damu hasa wakati wa kujisaidia. matibabu yanategemea aina na hatua ya ugonjwa. Ila ni vizuri ukamwona Daktari akakushauri zaidi kulingana na tatizo lako. ushauri wangu, ni vizuri kula vyakula vyenye roughage, kula matunda, kunywa maji mengi, kutumia maji (hasa ya vuguvugu) kujisafisha baada ya haja kubwa, na kujiepusha na visababishi vyote nilivyovitaja hapo juu.
wako Dr. ismase