Tatizo wewe mgeni ulikuja na mihemko hukujua huku kuna ustaarabu wake, ukajidanganya wewe ndiye mwenye dhamana ya kuwatusi watu, kwamba wengine hatujui jinsi ya kutukana, kwa taarifa yako mimi hapa nimewahi kula ban kwa ajili ya matusi makubwa hata zaidi ya wewe ambaye bado unajifunza.
Pambanua na kupangua hoja za wadau, wote tunakutana huku kama wana Afrika mashariki, japo utaona tukishindana humu udhani tuna chuki, lakini nje kwenye kazi zetu tuashirikiana sana hatuna chuki. Hawa Watanzania unaowaona humu wengi wapo Kenya wanapiga mishe, vile vile kuna Wakenya humu huja huko Tanzania.
Tunachofanya ni kusogeza muda kwa ushindani wa kindugu lakini sote tunahitajiana kwa namna moja au nyingine.