LEVEL
Senior Member
- Jul 4, 2013
- 195
- 51
jana nilikua mmoja kati ya wajumbe walioshiriki uzinduzi wa rasimu ya pili ya katiba ya tanzania uliofanyika chuo cha mipango dodoma tarehe 8.03.2014. Chakushangaza kilichofanyika ni kusikiliza hotuba zisizokua na maana huku siku hiyo mhimu sana ikiunganishwa na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hivyo kusababisha muda wa kutoa michango inayohusu uundwaji wa katiba kuwa mfupi mno. kutokana na hilo nimejiuliza maswali yafuatayo
1. kama uzinduzi wa rasimu ya pili kanda ya kati dodoma umefanywa kizembe kiasi hiki je? wale wenzetu waishio vijijini watakua na mchango gani katika katiba ya nchi yao.
2.kwanini serikali inafanya masiara katika kuandaa katiba ambayo ni chombo mhimu sana katika kuongoza nchi yetu.
3. kwanini muda uliotolewa katika uchambuzi wa rasimu ya pili ni mfupi na hivyo kufanya wananchi kushindwa kutoa maoni yao katika swala zima la uundwaji wa katiba.