Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Tatizo ni kuwa uchungu wa posho kwa wabunge au wizi wa fedha a umma hausikiki kwa Watanzania wengi. Yawezekana wapo wanaona haya ni mambo mabaya kiakili tu lakini si kimaadili. Mtu ambaye na yeye huku ngazi za "chini" anaishi kimitkasi, kujitengenezea vitrip vya hapa na pale na hata kutumia nafasi yake na yeye "kujineemesha" anaweza vipi kuwa na uhalali wa kuona ubaya wa posho au mambo haya. Hivi kweli tunaamini kama mianya ya watu kujitengenezea pesa kwenye nafasi zao ikizibwa kweli kuna watu wataishi na kufanya kazi kweli? Au tunachukia kwa sababu hawa wabunge wanafanya wazi kabisa kile ambacho watu wengine wanakifanya kwa siri siri?
Au watu wanawaonea wivu hawa kwa vile wamethubutu na wanaweza? Kwamba wakati watu wengine wanapotaka kujichotea 'vijisenti' inabidi watumie mbinu nyingi za kalamu na haramu ili waweze kuficha dhambi zao lakini wenzetu hawa bila haya wala hiyana wanaweza kujaribu kutengeneza posho; fikiria kuna posho ya madaraka!