Kuna dada mmoja nafanya naye kazi ni mjamzito, amekuwa msahaulifu sana. Mnaweza kuongea jambo leo kesho itakubidi uanze upya kumkumbusha hali hiyo inanikwaza sana. Wakati mwingine hata simu yake anaweza kusahau kaweka wapi kwa muda mfupi tu, cha ajabu huweza hata kusahau fedha mfano km umemwazima au kamtuma mtu kitu asipokumbuka kumrudishia chenchi basi ataanza kutafuta alikoweka hela.
Naomba kuelimishwa, je hili tatizo linasababishwa na nini?......:confused2: