Ni ujinga,ulimbukeni na ushamba kusifia chuo unachosoma na kuviponda vingine!

The_Emperor

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2012
Posts
871
Reaction score
125
Ni kwa kipindi sasa naona mijadala ya vyuo imekuwa ikishamiri humu jukwaani.Baadhi ya watu wamekuwa wakichangia upumbavu tu ingawa wanajiita wasomi,mara wanajisifiasifia wanapopatia elimu zao na kukejeli vyuo vingine.
Nakwambia hivi,dunia hii haina kanuni,na usijaribu kuipa kanuni,Mungu pekee ndiye anayeijua!
Kwa nini ujisifie chuo wakati kichwani kwako kumejaa ulimbukeni?Kwa nini ujisifie chuo wakati huwezi hata kucompete kwenye Soko la Afrika Mashariki?Acheni ushamba,mnaingia vyuoni hata perfect tenses hamjui halafu mnabishana humu ndani!
 
Hicho ni kidonge tayari Mkuu umeshawapatia, wakimeza wakitema ni shauri yao...
Hata bahari ya damu haiwezi kuuzamisha ukweli...
Tuache ushabiki wa majina ya vyuo...twendeni sokoni/field tuone nani anafanya kazi kwa ufanisi zaidi...
Tabia ya kusifia majina ya vyuo ndiyo yaliyoifikisha Tanzania mikononi mwa mafisadi...maana vyuo vyenye
kusifiwa kuwa ni bora zaidi ndimo walimosomea hao wengi wa mafisadi......
 
Pole kiongozi kwani wakijisifia wewe si uwaache tu ni nini kinakuharibia siku yako, hata wakijisifia walisoma mbinguni so what si uwaache. Kuliko kupandisha mori kiasi hiki lol
 
Kati ya hao waliojisifia, na wewe, nani mpumbavu kumshinda mwenzake? Mwenye akili akivuliwa nguo na mwendawazimu huchutama ila mpumbavu hufukuzana naye. Sasa kilichokukera wewe kiasi cha kuamua kuanzisha taarabu hapa ni kitu gani? Kama siyo inferiority complex tu ulizonazo kutokana na kusoma chuo cha kata?
 
Hivi Kichaa akipita wakati unaoga mtoni, achukue nguo zako aanze kukimbia nazo halafu wewe umfukuze huku ukiwa uchi, watu wakapoona hizo mbio, watafahamu kuwa ni nani kichaa baina ya yule unayemfukuza akiwa amevaa nguo au wewe unayemfukuza ukiwa uchi ?
 
Wanafunzi UDSM wanajiuza ili kukidhi Maisha.
Source. Mwananchi jana
 
Pole kiongozi kwani wakijisifia wewe si uwaache tu ni nini kinakuharibia siku yako, hata wakijisifia walisoma mbinguni so what si uwaache. Kuliko kupandisha mori kiasi hiki lol

Darasa huru,shule ya bure!Amkeni mliolala!
 

Pole sana kwa kumaliza vidato bila kuelimika!Nitajie hizo kata za hivyo vyuo!
 

Saa zengine una akili mdogo wangu, mpk mimi mkubwa wako nasikia raha. Sasa haka kadude ka kugongea LIKE kameganda sijui na kenyewe kamesoma KATA SCHOOL kwa hiyo kanakuonea wivu mwanawane
 

Mtoto wa UDOM ana hasira sana huyu!, kachungulie kwenye zile 100 bora kama ipo!, soma dogo acha kupoteza muda na watu hapa, wengi tunalipa kodi hapa hatuishi kwa boom! Shauri yako.
 
Ni jambo zuri kukikubali Chuo ulichosoma lakini inapokuja suala la ubora elimu au maarifa uliyopata hiyo ni zaidi ya jitihada ya mwanafunzi binafsi. Mtazamo wangu ubora wa mtu upimwe kwa uwezo wake binafsi, mara nyingi wasomi wachovu ndo huwa wanatafuta hifadhi ya kuficha ukilaza wao kwa kujiliwaza chuo alichosoma. Kama mtu uko makini wadau huwa hawaulizi huyu kasoma wapi bali wanakukubali ww kama ww.
 

asante sana... text sent.
 
Duh!humu,watu wana inferiority complex na vyuo vyao wanavyosoma.
 
Pole kiongozi kwani wakijisifia wewe si uwaache tu ni nini kinakuharibia siku yako, hata wakijisifia walisoma mbinguni so what si uwaache. Kuliko kupandisha mori kiasi hiki lol

point taken,,inaonekana hujasoma (ward university )
 
Mtoto wa UDOM ana hasira sana huyu!, kachungulie kwenye zile 100 bora kama ipo!, soma dogo acha kupoteza muda na watu hapa, wengi tunalipa kodi hapa hatuishi kwa boom! Shauri yako.

hahahahaaaa,,,,,,watasema unawanyanyasa wanafunzi........wengine hela zao ndo zitajenga daraja la kigamboni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…