Ni ukweli usiopingika kuwa gharama ya maisha imeongezeka sana na kuna malalamiko kila kona. Mitaani watu wanalaumu . Ni kweli vita vya Urusi dhidi ya Ukraine ndo imepandisha bei kwa kiasi fulani kama ingependeza Mhe. Rais angejitokeza hadharani kwenye vyombo vya habari kuelezea athari ya kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali. Watu wana chuki sana na gharama kupanda kila kukicha lakini hakuna maelezo yeyote kutoka kwa Mamlaka inayoweza kupoza wananchi.