Ni ukweli usiopingika kuwa gharama ya maisha imeongezeka sana

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Ni ukweli usiopingika kuwa gharama ya maisha imeongezeka sana na kuna malalamiko kila kona. Mitaani watu wanalaumu . Ni kweli vita vya Urusi dhidi ya Ukraine ndo imepandisha bei kwa kiasi fulani kama ingependeza Mhe. Rais angejitokeza hadharani kwenye vyombo vya habari kuelezea athari ya kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali. Watu wana chuki sana na gharama kupanda kila kukicha lakini hakuna maelezo yeyote kutoka kwa Mamlaka inayoweza kupoza wananchi.
 
Gharama za Maisha hazijapanda leo wala jana ni muendelezo tu..

Mara moja hii mmesahau kama mlipigwa biti hadi kusema neno “ vyuma vimekaza


Izo nguvu unazo tumia kwa Malalamiko, jibidiishe kutafuta kipato ufikie Uhuru wa kutumia.. Utakuja kunishkuru
 
Ni lini gharama za maisha zilipungua?
 
Jamani maisha yamekuwa ghali Sana,
Jalibu kuangazia bidhaa muhimu ambazo hazihusiani mojakwamoja na Vita vya Russia na Ukraine, mfano
-mafuta ya kupikia
- unga wa sembe
-vifaa vya UJENZI

Haya ni baadhi ya Mambo yanayopandikiza chuki ya wananchi dhidi ya mkuu wa nchi,ambapo mkuu wa nchi anaweza kutamka chochote kwa lengo la kuwafariji wananchi wake kama mpango wa mwezetu Rais wa France Emmanuel Macron. Kwa hali ya maisha kwa Sasa Rais anatakiwa kutoa kauli ya kuwafariji watanzania


Tanzania inakua ni nchi ambayo kuielewa inachukua mda kidogo hasa hapa ambapo nauli zimeshapanda anagali chombo kinachotakiwa kupanga nauli bado hakija kaa kujadili ni kiasi gani Cha fedha ya nauli kinatakiwa kuongezeka[emoji31][emoji31][emoji31][emoji31]
Kuna Mambo mengi yanaumiza Sana nchi hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…