Ni umri gani kisheria au ni aina gani ya elimu mzazi anawajibika kumsomesha mtoto?

Tatetitotu

Member
Joined
Mar 6, 2018
Posts
58
Reaction score
42
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Ningependa kupata ufafanunuzi wa kisheria kuhusu umri wa mtoto ambao mzazi anakuwa anawajibika msomesha mtoto na aina ya elimu kwani nina mtoto wa marehemu dada yangu nimemsomesha kwa shida elimu ya O'level ili hali baba yake mzazi yupo hai matokeo yanaonyesha uwezekano wa kuchaguliwa serikalini haupo lakini anaweza soma chuo au private (advance) umri wake ni miaka 19.

Je, sheria inawezatumika imbane baba yake amsomeshe sababu uwezo wa kufanya hivyo anao na mimi uwezo wangu ni mdogo?
 
Sheria ya Mtoto No. 21 ya 2019 kuhusu malezi ya mtoto inasema inasema ''until he is gainfully employed'' tafsiri yake inaweza kuwa ni hadi pale atakapokuwa ameajiriwa/ameweza kujiajiri.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Ningependa kupata ufafanunuzi wa kisheria kuhusu umri wa mtoto ambao mzazi anakuwa anawajibika msomesha mtoto na aina ya elimu kwani nina mtoto wa marehemu dada yangu nimemsomesha kwa shida elimu ya O'level ili hali baba yake mzazi yupo hai matokeo yanaonyesha uwezekano wa kuchaguliwa serikalini haupo lakini anaweza soma chuo au private (advance) umri wake ni miaka 19.

Je, sheria inawezatumika imbane baba yake amsomeshe sababu uwezo wa kufanya hivyo anao na mimi uwezo wangu ni mdogo?
umeshindwaje ku-face baba yake ili amsomeshe na je kuna mazingira gani yanayomfanya asimsomeshe? weka wazi tukupe mawazo Je alikuwa ni mtoto wa ndoa au alikuwa ni wa nje kwa huyo baba?
 
Kwa kifupi ni mtoto wa nje na dada amefariki akiwa hata darasa la kwanza ajanza kabla ya dada kufariki alionyesha kumjali lakin baada ya kufariki hakuwahi mjali kwa namna yoyote ile, shule ya msingi Babu yake kwa kiasi kikubwa ndo alimsomesha baada ya baba ake Kayla fanya hivyo shule ya sekondari nilichukua jukumu hilo baada ya juhudi zote za kumuomba baba ake asaidie bila mafanikio yaani alikataa kwa madai pia anawatoto wengine wakusomesha na kwamba hilo jukumu ni letu sote kama naweza nifanye kama siwezi basi asisome nilijitahidi akasoma mpaka akamaliza lakini kwa sasa uwezo wangu wa kiuchumi ni mbaya sana na natamani mwanangu aendelee na masomo
 
Nenda kawaeleze watu wa ustawi wa jamii walioko karibu watakueleza njia za kufanya ili abananishwe
 
Hii kitu inamuumiza sana mtoto,

naweza image ni jinsi gani mtoto anateseka kisaikolojia,

kwamba ana watoto wengine wa kusomesha maana yake huyo mtoto hana thamania hata kidogo

kibaya zaidi huenda huyo baba heshima yake mtaani ni kubwa kuliko

niwahi ona hiyo kwamba baba anamwambia mtoto subiri wenzako wamalize kwanza wakati wana umri sawa

Hii ni roho mbaya iliyopitiliza aisee
 
Back
Top Bottom