Ni upi ukweli kuhusu Nguva (Samaki mtu)?

Mimi nimesoma wildlife nilipokuwa chuo, lkn tunamsoma Nguva kama mnyama anaeishi katk maji na haswa baharini, na mtu alie eneza uvumi huu alikuwa ni Christopher Columbus aliegundua bara la America ndo alisema akiwa safarini ktk bahari alionana na samaki mtu mara 3, hapo ndo ikaanza dhana nzima ya uwepo wao, lkn hakuna mpaka leo sehemu yeyote duniani walipoweka kumbukumbu ya mwili wake zaidi ya picha na filamu za kufikirika, Nguva sio samaki mtu, ukienda pale makumbusho ya taifa ya hapa kwetu Dar es salaam unamkuta nguva yupo lkn sio samaki mtu, ni mnyama na hata hafanani na binadamu
 
Hata Mimi inanichanganya, niliongea na mtaalam mmoja yeye alisema hakuna samaki kama huyo kabisa, japo nguva yupo ila ni samaki wa kawaida, baada ya tsunami Indonesia tulirushiwa picha ya nguva dume mzee nusu mtu na kama miezi miwili hivi iliyopita yaani Decemba kuna picha nyingine ilikuwa inarushwa kwenye WhatsApp kapatikana mwingine kama sikosei ni somalia na huyu alikua mzima sasa sijui niamini lipi. Na bado wataalamu wengi wa samaki hawakubaliani na hiyo ya nusu mtu
 
Kwani vipande vya samaki vinavyouzwa mitaani vikiwa kwenye kikabati chenye vioo ni aina gani ya samaki?
 
Huyu samaki yupo kama huamini nenda kawaulize wa vuvi, kuna baadhi walisha bahatika kuwaona viumbe hawa.
 
Huyu anaesemekana amekutwa kafa ni nguva wa kutengeneza na jamaa mmoja mmarekani na alihojiwa akakiri na mpaka siku moja kwenye kipindi cha clouds 360 walimuonesha jamaa kwenye kiwanda chake cha kutngeneza mazombie na madude kama hayo.
 
SAMAKI ANAJUA SALUNI!
 
Huyu ndie mnyama wa baharini ambae wavuvi humuita nguva, hawa wanyama ni wapole na wanakula majani, wapo aina mbili dugong wapo indian ocean na east africa msumbiji hadi misri
. na manatee wapo west africa na caribean, mexico. Hakuna mnyama ambe ni nusu mtu nusu samaki....ni hadithi. ila wavuvi wetu hukutana dogong

Huyu chini ni dugong












manatee


Tofauti zao
 
Huu ndo ukweli
 
Duh!Hahaha!Nimecheka sana.Eti nyani ni wengi sana Africa!Haya basi kale ndizi na mapapai!
 

Ebu tujaribu kuangalia hizi video mbili za kwanza tuone kama kuna uhalisia kuwa hivi viumbe ni kweli vipo? au na hizi video ni za kutengenezwa?


 

Mkuu Pasco ebu angalia hizi video, kwa kuwa wewe ni mtaalamu je ni halisi au zimetengezwa? kwa kuangalia huyo kiumbe aliyepo kwenye mwamba baharini na huyo anayejirusha kutoka majini na kuzama tena.

 
Nashindwa nifwaate msimamo upi kuhusu hawa viumbe , hadidhi zao nimezisikia toka utoto nahata bibi yangu alisha nihadthia uwepo wahaya madubwasha nashindwa kuelewa huyu mtualie eneza uzushi wa uwepo wahawa samaki nusu mtu nusu binadamu , alifanikiwa vipi kuu danganya ulimwengu mzima.

Mimi nina hisi huenda hapo zamani walikuwepo alafu wakatoweka, maana,siamini kwamba kila mtua angeweza kudanganyika kwa wakati wote huo , siamini kama video zoote tunazo ziona nizaku tengenezwa , haini ingii akilini kwamba huu ni uwongo ulio zushwa kwenye dunia nzima bila hata ya vitabu , bibi ya ngualiawahi kuniambia kuna kiji sehemu ambacho huitwa NGUVENI nanina kijua kwamba chanza, chaeneo hilo kuitwa hivyo nikutokana na zamani alikuwa akionekana samaki ambaye ana Sura na kifua chamtu , yaani NGUVA . Nashindwa kuelewa kama kuna mvumishaji alianza lini huo uvumi paka ukaenea,kipindi bibi yangu mwenye umri wa miaaka 90 ausikie akiwa binti , haini ingii akilini.
 
Ebu tujaribu kuangalia hizi video mbili za kwanza tuone kama kuna uhalisia kuwa hivi viumbe ni kweli vipo? au na hizi video ni za kutengenezwa?


Kiutafiti au sayansi- hakuna kiumbe kama huyo baharini Labda kiimani...asa ni wewe binafsi mkuu uko upande upi. mimi nipo team sayansi. na kwakusikiliza stori za nguva na kufatilia wasemavyo watafiti katika marine biology kilichoaminika wavuvi wa east africa hukutana na dugong ambae wanamwita nguva.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…