Ni upi utaratibu wa Kisheria kubadili majina?

Ni upi utaratibu wa Kisheria kubadili majina?

2sexy

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2020
Posts
682
Reaction score
1,529
Habari zenu wakuu,

Naomba kujulishwa natakiwa nifanyeje ili niweze kubadili majina ya vyeti vya kitaaluma pamoja na kitambulisho cha Nida ambavyo vinasoma tofauti.

Mfano mimi naitwa Neema Yusuph Ibrahimu ;Majina haya yanatokea kwenye cheti cha kuzaliwa na nida.

Ila vyeti vya kitaaluma vyote vimeandikwa Neema Y Ibrahimu. Natakiwa kufanyaje kubadili majina haya na gharama zake zipoje.

Ahsanteni
 
Hapo kubadilisha ni nida tu ili vifanane na vyeti vyako.
Shida ni cheti cha kuzaliwa, ndio tatizo linapoanzia
Je nikifika NIDa na cheti hikohiko tatizo si bado litakuepo, au mpk nifanye utaratibu wa kubadilisha jina kwenye cheti cha kuzaliwa ?
 
Nenda kwa mwanasheria atakuandikia kitu kinaitwa Deed Poll,then utaenda kwa kamishna wa viapo unalipia 35k nadhani..hiyo deed poll utakuwa unaiambatanisha pamoja na documents zako zote hizo,in case unataka kuzitumia
 
Habari zenu wakuu,

Naomba kujulishwa natakiwa nifanyeje ili niweze kubadili majina ya vyeti vya kitaaluma pamoja na kitambulisho cha Nida ambavyo vinasoma tofauti.

Mfano mimi naitwa Neema Yusuph Ibrahimu ;Majina haya yanatokea kwenye cheti cha kuzaliwa na nida.

Ila vyeti vya kitaaluma vyote vimeandikwa Neema Y Ibrahimu. Natakiwa kufanyaje kubadili majina haya na gharama zake zipoje.

Ahsanteni
Fanya hivi
Uandaliwe deed poll ya majina
Ipeleke wizara ya ardhi ukasajiri 32000
Peleka kwenye gazeti la serikali kutangazwa 20000
Peleka nida 20000
Hapo utakuwa umekamilisha

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom