Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Habari za wakati huu waungwana wa JF.
Kutokana na hali ilivyo kwa sasa nchini, imeniwia vigumu kuelewa na kupata maana halisi ya neno uzalendo.
Kumekuwa na makundi mawili ya watu, wale wanao fukua na wale wanao fukia maovu.
Wengi tunajua uzalendo ni hali au tabia ya kuonyesha mapenzi au kujali mambo ambayo yanalihusu taifa husika. Ni kweli kwamba sisi kama watanzania, tunapaswa kuipenda na kuitetea nchi yetu.
Katika kuitetea nchi yetu, ni vyema kujali na kuonyesha mapenzi ya kweli kwa kukemea na kusema ukweli pale ambapo mambo hayaendi vizuri.
Kutokana na hali hii, jambo linalo nishangaza hasa ni pale mtu anapo kosoa au kusema ukweli (kufukua) juu ya machafu yanayo fanyika, kutetea haki na maslahi ya wananchi, mwisho mtu huyo ataambiwa yeye sio mzalendo.
Watanzania wengi wanaamini uzalendo ni kutetea tu (Kufukia) na kutoruhusu mtu mwingine kusema au kukosoa utawala au viongozi ambao wana nafasi za juu katika utawala.
Kwangu uzalendo wa kweli kabisa unaanzia ndani ya moyo wa mtu na sio mdomoni, kama unapata uchungu na maumivu kutokana na kuona nchi inaelekea pabaya, ukasimama na kusema ukweli, basi huo ndiyo uzalendo wa kweli.
Wakosoaji wengi wamekuwa wa wakipewa lawama kwamba wao wanakosa uzalendo pamoja na kuhatarisha amani na utulivu wa nchi. Watanzania wengi wana amini kwamba mzalendo wa kweli
ni yule anayesema mazuri tu au kusifia mambo mbalimbali katika nchi au uongozi husika.
Watanzania tunapaswa kurejea na kuanza kutafuta maana halisi ya uzalendo, sio tu kuvaa bangili yenye bendera ya taifa na kujiona tayari ni mzalendo. Kufukia maovu na kuogopa kuwakosoa viongozi huo sio uzalendo pia.
Kufukia maovu kwa kuogopa maneno kwamba eti amani au utulivu wa nchi utapotea ni dalili mojawapo ya kukosa uzalendo wa kweli.
Mdauu, wewe upo kundi gani, unafukia au unafukua?
Personally, I prefer dangerous freedom over peaceful slavery.
#BM