Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Katika uchaguzi huu uliopita wa 2020, CHADEMA walitegemea sana nguvu ya Mwanamke.
Cha kushangaza, CCM ambao kwa miaka mingi walituaminisha kuwa Mwanamke wa Kitanzania ana ushawishi mkubwa katika siasa zetu, walionekana kutojali kabisa nguvu ya Mwanamke, labda Zuchu tu.
Wagombea Wanawake nafasi ya Ubunge kwa CCM walikuwa wachache na hakukuwa na juhudi zozote za kusafisha kauli za ukakasi za kiongozi wao dhidi ya Wanawake.
Cha kustaajabisha kingine, binafsi sikuona juhudi au mbinu zozote za kiubunifu za CHADEMA kumobilize Mwanamke wa Kitanzania katika uchaguzi huu, zaidi ya kuweka wagombea wengi kwa nafasi ya Ubunge. Kuna jambo halikuwa sawa ndani ya chama.
Juzi nilileta mada nyingine niliyoomba tujadili mada ya maslahi ya Taifa. Ni watu wa wachache sana wenye uwezo wa kukataa, wakiambiwa wafanye jambo fulani kwa maslahi ya taifa, hata kama litaleta ukakasi kwa wale wanaowazunguka.
Nisiseme mengi. Nimeokota hii clip sehemu, nimeone niitupie hapa iambatane na bandiko langu.