SoC02 Ni usawa au kufanana kijinsia?

SoC02 Ni usawa au kufanana kijinsia?

Stories of Change - 2022 Competition

Konny Joseph

Senior Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
118
Reaction score
199
Usawa wa kijinsia ni lengo la jitihada za kuleta usawa katika jinsia zote,kutokana na dhulma mbalimbali za jinsia moja dhidi ya nyingine.Usawa wa kijinsia unahusiana na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na maendeleo ya kiuchumi.

Hoja hii imejengwa juu ya msingi kwamba kwa vile heshima ya binaadamu ni sawa kwa mwanaume na mwanamke, hivyo lazima wote wapate haki zinazofanana bila kujali majukumu na asili yao katika maisha.

Hapana shaka, utu na heshima yao ni sawa kwao wao wote; wote wanapaswa kuwa na haki sawa. Lakini swali la msingi tunalopaswa kujiuliza ni vipi kuhusu kufanana kwa haki zao?

Ikiwa badala ya kufuata kibubusa mawazo ya Kimagharibi tutaamua kufikiri sisi wenyewe kwa misingi thabiti ya desturi zetu, swali la kwanza linalokuja akilini ni iwapo kweli haki sawa zinamaanisha haki zinazofanana. Kwa kweli hayo ni mambo mawili tofauti.

Usawa ni haki ya kuwa na daraja sawa kithamani na hadhi ambapo kufanana maana yake ni kulandana. Inawezekana baba akagawa mali zake kwa watoto wake watatu kwa usawa lakini sio kwa kulingana.

Jaalia mali yake inajumuisha vitu mbali mbali kama vile maduka, mashamba na badhi ya mali zilizokodishwa. Baba kwa kuzingatia vipaji vyao na mambo ambayo kila mmoja anapenda, anaamua kumpa mmoja duka, mwingine shamba na wa tatu mali zilizokodishwa.

Anazingatia kuwa thamani ya mali aliyopewa kila mmoja wao ni sawa na wengine na kila mmoja amepewa kutokana na kipaji chake. Hivyo aligawa mali yake kwa usawa lakini sio kwa kulingana.

Uwingi ni tofauti na ubora, na usawa ni tofauti na kufanana.Jamii ya kitanzania inapaswa kutokuamini juu ya kulingana (uniformity) kwa mwanaume na mwanamke.Lakini wakati huo huo isiwapendelee wanaume katika maswala ya haki.Jamii lazima izingatie kanuni ya usawa kati ya mwanamke na mwanaume lakini isikubaliane na kufanana kwa haki zao.

Hapana shaka kuwa asili ya maisha ya binadamu haijatoa haki zinazofanana kati ya mwanaume na mwanamke katika mambo yote. Lakini pia haijaamuru majukumu na adhabu zinazofanana kwa jinsia hizi mbili. Yote kwa yote ni kuwa thamani ya jumla ya haki za mwanamke sio ndogo kuliko ile ya mwanaume.

Hapa linazuka swali, kwa nini haki za mwanaume na mwanamke hazijafanana katika mambo yote. Jibu la jumla ni kwamba asili ya kimaumbile ya mwanamke naq mwanamme haitaki wafanane. Nafasi hii inataka wasifanane katika haki nyingi, majukumu, wajibu na adhabu.

Hapa ndio kuna tofauti kati ya mtazamo wa desturi zetu na mfumo wa Kimagharibi katika nchi yetu, nukta inayobishaniwa ni suala la kufanana kwa haki sio usawa wa haki kati ya mwanamke na mwanaume.

Usawa wa haki ni nembo tu ambayo imewekwa kwa makosa katika zawadi hii ya Kimagharibi.Lakini lengo hasa linalotakiwa na wamagharibi ni kufanana au kulandana kwa haki baina ya jinsia hizi mbili.

Na ndio maana katika kuipigania dhana hii juhudi kubwa imeelekezwa katika kuhakikisha mwanamke na mwanamme wanafanana katika mambo yote.Ndio maana kupitia dhana hii kunaibuka haki ya ndoa za jinsia moja ili kusudi mwanamke ambae kiasili anastahiki kuolewa awe na jukumu na uwezo kuoa na mwaname mwenye jukumu na uwezo wa kuoa awe na haki ya kuolewa.

Na hata katika ndoa ya mwanamke na mwanamme, kumekuwa na jitihada ya kupandikiza dhana kwamba mume na mke lazima wawe na haki zinazofanana ndani yake.Hii ni kusema kwamba hakuna atakae kuwa na mamlaka ya kumuongoza mwengine, wala mwenye jukumu la kutii matakwa ya mwengine.

Dhana hii imekuwa sumu kubwa katika mahusiano ya kindoa katika dhama za sasa kwa kuwa imekuwa inakwenda kinyume na matakwa ya kimumbile yanayomtaka mwanaume kuwa kichwa na kiongozi wa familia na kumtaka mwanamke kuwa mtii na msikivu kwa mume wake ili kujenga msingi bora wa kifamilia.

Ni moja ya tofauti kati ya hulka ya nchi za Mashariki (Asia) na zile za Magharibi. Nchi za Mashariki zinazingatia maadili na za Magharibi zinazingatia haki.

Mtu wa Mashariki ana upendo zaidi na anaamini kuwa lazima asamehe awe na moyo wa ubinadamu. Lakini mtu wa Magharibi anaamini kuwa kama binadamu lazima azijue na kuzilinda haki zake na lazima asiruhusu wengine wazipore.

Utu unahitaji maadili na haki pia. Utu unahusiana na haki na maadili. Moja tu katika hizi haitoshi kuwa kigezo cha sifa bora za binadamu.

Hivyo kujenga dhana pekee ya kutaka haki bila kuzingatia maadili hakuwezi kumwelwkwza mtu au jamii katika mwelekeo mwema,kama ambavyo kusimamia maadili tu bila haki au sheria hakuwezi kuzaa matunda yalio mema.

Kimsingi hatupaswi kupinga jitihada za kuleta ustawi na maendeleo ya jinsia zote katika jamii, lakini jitihada hizo zisiwe kupitia kuzifanya jinsia mbili hizi zifanane au zilandane katika haki na ,majukumu yao.Ni vyema kila mmoja kati yao kusimama na kubaki katika nafasi yake ili kuleta mgawanyo bora wa majukumu,misingi bora ya kimaadili,na kuheshimiana.

Hivyo ni vyema kwetu sote kuamini kuwa kutofanana kwa haki kati ya mwanaume na mwanamke, kwa mujibu wa mipaka ya maumbile na tofauti zao ndio kutenda haki zaidi. Hukidhi mahitaji ya haki za asili vizuri zaidi, hutoa hakikisho kwa furaha ya familia na huisukuma jamii mbele katika njia ya maendeleo bora zaidi.
 
Upvote 1
Usawa wa kijinsia ni lengo la jitihada za kuleta usawa katika jinsia zote,kutokana na dhulma mbalimbali za jinsia moja dhidi ya nyingine.Usawa wa kijinsia unahusiana na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na maendeleo ya kiuchumi.

Hoja hii imejengwa juu ya msingi kwamba kwa vile heshima ya binaadamu ni sawa kwa mwanaume na mwanamke, hivyo lazima wote wapate haki zinazofanana bila kujali majukumu na asili yao katika maisha.

Hapana shaka, utu na heshima yao ni sawa kwao wao wote; wote wanapaswa kuwa na haki sawa. Lakini swali la msingi tunalopaswa kujiuliza ni vipi kuhusu kufanana kwa haki zao?

Ikiwa badala ya kufuata kibubusa mawazo ya Kimagharibi tutaamua kufikiri sisi wenyewe kwa misingi thabiti ya desturi zetu, swali la kwanza linalokuja akilini ni iwapo kweli haki sawa zinamaanisha haki zinazofanana. Kwa kweli hayo ni mambo mawili tofauti.

Usawa ni haki ya kuwa na daraja sawa kithamani na hadhi ambapo kufanana maana yake ni kulandana.

Inawezekana baba akagawa mali zake kwa watoto wake watatu kwa usawa lakini sio kwa kulingana.

Jaalia mali yake inajumuisha vitu mbali mbali kama vile maduka, mashamba na badhi ya mali zilizokodishwa.

Baba kwa kuzingatia vipaji vyao na mambo ambayo kila mmoja anapenda, anaamua kumpa mmoja duka, mwingine shamba na wa tatu mali zilizokodishwa.

Anazingatia kuwa thamani ya mali aliyopewa kila mmoja wao ni sawa na wengine na kila mmoja amepewa kutokana na kipaji chake. Hivyo aligawa mali yake kwa usawa lakini sio kwa kulingana.

Uwingi ni tofauti na ubora, na usawa ni tofauti na kufanana.Jamii ya kitanzania inapaswa kutokuamini juu ya kulingana (uniformity) kwa mwanaume na mwanamke.Lakini wakati huo huo isiwapendelee wanaume katika maswala ya haki.Jamii lazima izingatie kanuni ya usawa kati ya mwanamke na mwanaume lakini isikubaliane na kufanana kwa haki zao.

Hapana shaka kuwa asili ya maisha ya binadamu haijatoa haki zinazofanana kati ya mwanaume na mwanamke katika mambo yote. Lakini pia haijaamuru majukumu na adhabu zinazofanana kwa jinsia hizi mbili. Yote kwa yote ni kuwa thamani ya jumla ya haki za mwanamke sio ndogo kuliko ile ya mwanaume.

Hapa linazuka swali, kwa nini haki za mwanaume na mwanamke hazijafanana katika mambo yote. Jibu la jumla ni kwamba asili ya kimaumbile ya mwanamke naq mwanamme haitaki wafanane. Nafasi hii inataka wasifanane katika haki nyingi, majukumu, wajibu na adhabu.

Hapa ndio kuna tofauti kati ya mtazamo wa desturi zetu na mfumo wa Kimagharibi katika nchi yetu, nukta inayobishaniwa ni suala la kufanana kwa haki sio usawa wa haki kati ya mwanamke na mwanaume.

Usawa wa haki ni nembo tu ambayo imewekwa kwa makosa katika zawadi hii ya Kimagharibi.Lakini lengo hasa linalotakiwa na wamagharibi ni kufanana au kulandana kwa haki baina ya jinsia hizi mbili.

Na ndio maana katika kuipigania dhana hii juhudi kubwa imeelekezwa katika kuhakikisha mwanamke na mwanamme wanafanana katika mambo yote.Ndio maana kupitia dhana hii kunaibuka haki ya ndoa za jinsia moja ili kusudi mwanamke ambae kiasili anastahiki kuolewa awe na jukumu na uwezo kuoa na mwaname mwenye jukumu na uwezo wa kuoa awe na haki ya kuolewa.

Na hata katika ndoa ya mwanamke na mwanamme, kumekuwa na jitihada ya kupandikiza dhana kwamba mume na mke lazima wawe na haki zinazofanana ndani yake.Hii ni kusema kwamba hakuna atakae kuwa na mamlaka ya kumuongoza mwengine, wala mwenye jukumu la kutii matakwa ya mwengine.

Dhana hii imekuwa sumu kubwa katika mahusiano ya kindoa katika dhama za sasa kwa kuwa imekuwa inakwenda kinyume na matakwa ya kimumbile yanayomtaka mwanaume kuwa kichwa na kiongozi wa familia na kumtaka mwanamke kuwa mtii na msikivu kwa mume wake ili kujenga msingi bora wa kifamilia.

Ni moja ya tofauti kati ya hulka ya nchi za Mashariki (Asia) na zile za Magharibi. Nchi za Mashariki zinazingatia maadili na za Magharibi zinazingatia haki.

Mtu wa Mashariki ana upendo zaidi na anaamini kuwa lazima asamehe awe na moyo wa ubinadamu. Lakini mtu wa Magharibi anaamini kuwa kama binadamu lazima azijue na kuzilinda haki zake na lazima asiruhusu wengine wazipore.

Utu unahitaji maadili na haki pia. Utu unahusiana na haki na maadili. Moja tu katika hizi haitoshi kuwa kigezo cha sifa bora za binadamu.

Hivyo kujenga dhana pekee ya kutaka haki bila kuzingatia maadili hakuwezi kumwelwkwza mtu au jamii katika mwelekeo mwema, kama ambavyo kusimamia maadili tu bila haki au sheria hakuwezi kuzaa matunda yalio mema.

Kimsingi hatupaswi kupinga jitihada za kuleta ustawi na maendeleo ya jinsia zote katika jamii, lakini jitihada hizo zisiwe kupitia kuzifanya jinsia mbili hizi zifanane au zilandane katika haki na ,majukumu yao.

Ni vyema kila mmoja kati yao kusimama na kubaki katika nafasi yake ili kuleta mgawanyo bora wa majukumu,misingi bora ya kimaadili,na kuheshimiana.

Back
Top Bottom