Ni utafiti gani ambao Tanzania tumewahi kufanya ukatambulika duniani?

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
21,600
Reaction score
35,158
Nimekaa nikawaza, leo nchi kama India, Japan, Urusi, Marekani zinapigana vikumbo kuingia mwezini!

Je, sisi Watanzania ni tafiti gani tumewahi fanya hapa duniani?

Je, katika bajeti ya serikali ni kiasi gani kimetengwa au kimewahi kutengwa kwa ajili ya tafiti?

NB: Naongelea tafiti ambayo serikali imefadhili na sio tafiti zinazofanywa kwa msaada wa watu wa Marekani.
 
Labda MKUKUTA!.... Teh teh teh!

... Eti mpango wa Kukuza Uchumi, na kupunguza umasikini Tanzania.....

Hii nchi bana...ina vichekesho...! Maigizo sijui yataisha lini!!?
 
Si unaangalia na hali halisi ya uchumi wa nchi yako halafu ndiyo unaanza kutoa challenges za namna hii?

Serikali ina watu inaohitaji kuwahudumia, na hivyo kwa sasa haina fedha ya ziada ya kuingia kwenye tafiti za aina hii. Ni maoni yangu, siisemei Serikali

NI mpumbavu tu anayeweza kuanza kufanya utafiti wa aina hii ilhali kuna watoto wanahitaji vyumba vya madarasa na baadhi ya wananchi wanahitaji chakula na mbolea ya ruzuku kutoka Serikalini

Ningekubaliana na wewe kama tuseme ungehoji kwamba kwa nini bado sisi hatujafikia hatua hiyo hadi muda huu na si kuanza ku-challenge kwamba kwa nini sisi hatufanyi utafiti wa aina hiyo
 
Mara nyingi tafiti zinafanywa na wasomi:-
  • Wanazuoni:- PhDs, Profs
  • Wanasayansi:- je tunao?
Wamefanya jitihada zipi, waliomba kuwezeshwa wakanyimwa?
 
Tuchape kazi....
Watanzania tusitishwe...
Haya ni mafua yalio changamka...
R.i.P John..😥
 
Hata hujaelewa mada.

Hayo ya mwezini nimetolea mfano.

Swali nililo uliza je ni tafiti gani hapa duniani ambayo imefanywa na watanzania?

Nilitarajia unitee list ya tafiti na sio kufocus kwenye mfano niliotoa.
 
Mara nyingi tafiti zinafanywa na wasomi:-
  • Wanazuoni:- PhDs, Profs
  • Wanasayansi:- je tunao?
Wamefanya jitihada zipi, waliomba kuwezeshwa wakanyimwa?
Hiyo ni mara nyingi. Tuchukulie hao wanazuoni hawajahi omba fund serikalini (japo si kweli) Je hao wengine wa "mara chache" wamefanya kipi?
 
Ugaidi na uhaini + usaliti!!
 
Utafiti na uvumbuzi sii kipaumbele ktk Taifa hili kwa sasa hivi eti unajenga shule na baabara ya sayansi wakati wanafunzi hawa wakimaliza chuo ajira wanasayansi sii kipaumbele! Kwa nini nomsomeshe mwanangu shule za sayansi na sii Accounts apate ajira fasta alete pesa nyumbani?
 
Pesa ya utafiti kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imetengwa shilingi ngapi tuanzie hapo
 
Hata hujaelewa mada.

Hayo ya mwezini nimetolea mfano.

Swali nililo uliza je ni tafiti gani hapa duniani ambayo imefanywa na watanzania?

Nilitarajia unitee list ya tafiti na sio kufocus kwenye mfano niliotoa.
Tunao wasomi wengi tu maDr na maProfessor na wote hawa wamefanya tafiti za kutosha kufikia kwenye level hizo. Au pengine labda unataka tafiti za aina gani hasa? Tuseme labda kama vile za kuunda chombo cha kwenda mwezini? Wewe ni msomi? Katika level gani?
 
Korona kushambulia mapapai na ugunduzi wa dawa ya kuvukiza na mashine kuwekwa muhimbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…