Ni utapeli au napoteza bahati?

Ni utapeli au napoteza bahati?

SubTopic

Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
95
Reaction score
175
Kisa Changu Kiko hivi, Kuna mzungu aliniomba urafiki Facebook baada ya kumkubalia akaniomba namba ya Whatsapp. Tukaanza kuwasiliana ndani ya siku mbili tatu akaahidi kunitumia mzigo ambao ni simu ya iPhone 16.

Yeye anaishi London uingereza na siku aliyotuma mzigo alisema kuwa amekosa ndege inayokuja moja kwa moja Tanzania hivyo akatuma kwenye ndege inayoishia Kenya maana walimwambia kuwa mzigo ukifika wanaweza kufanya delivery uwanja wa ndege ulio karibu (hapahapa East Africa).

Basi bwana yule mzungu akatuma mzigo na akanitumia picha ya mzigo pamoja na risiti na zote Zina majina yangu maana aliniambia nimtumie majina yote matatu na namba ya simu, na akaniambia mzigo utafika Nairobi baada ya masaa 9 na akanisisitiza kuwa niwe Makini na muda kwani mzigo ukishafika watanijulisha na kweli baada ya masaa Tisa (mzigo aliutuma saa 2 usiku saa 11 ukawa umefika Jomo Kenyatta Airport Kenya).

Wale jamaa wa airport wakanipigia wakaniambia kuwa Kuna mzigo wangu wameupokea kutokea uingereza na umeshalipiwa Kila kitu ni Mimi kwenda na kitambulisho Changu tu nikauchukue.

Nikawaambia Mimi sipo Kenya nipo Tanzania Kama wanaweza kuutuma wautume. Kwa sehemu niliyowaambia wakasema inagharimu shilingi 125,000 ili mzigo ufike uwanja wa ndege niliopo.

Wamenionesha na picha ya mzigo kabisa ndio ule uliotumwa Kule uingereza. Sasa najiuliza hii kitu imekaaje? Maana wao wanasema mzungu kalipia mzigo mpaka pale ulipofikia Ila hizo gharama za kuja huku Tanzania ni gharama nyingine kwakuwa mzigo unatakiwa kukatiwa ticket na hiyo ni gharama ya ticket.

Na njia ya malipo wamesema naweza kutumia mpesa au Tigo pesa. Ndo najiuliza hapa nitumie au nakaribia kutapeliwa? Maana Sina uzoefu na upokeaji wa mizigo iliyotumwa kutokea nje ya nchi.

Nawasilisha wakuu. Naombeni ushauri wenu.
 
Kisa Changu Kiko hivi, Kuna mzungu aliniomba urafiki Facebook baada ya kumkubalia akaniomba namba ya Whatsapp. Tukaanza kuwasiliana ndani ya siku mbili tatu akaahidi kunitumia mzigo ambao ni simu ya iPhone 16. Yeye anaishi London uingereza na siku aliyotuma mzigo alisema kuwa amekosa ndege inayokuja moja kwa moja Tanzania hivyo akatuma kwenye ndege inayoishia Kenya maana walimwambia kuwa mzigo ukifika wanaweza kufanya delivery uwanja wa ndege ulio karibu (hapahapa East Africa). Basi bwana yule mzungu akatuma mzigo na akanitumia picha ya mzigo pamoja na risiti na zote Zina majina yangu maana aliniambia nimtumie majina yote matatu na namba ya simu, na akaniambia mzigo utafika Nairobi baada ya masaa 9 na akanisisitiza kuwa niwe Makini na muda kwani mzigo ukishafika watanijulisha na kweli baada ya masaa Tisa (mzigo aliutuma saa 2 usiku saa 11 ukawa umefika Jomo Kenyatta Airport Kenya)
Wale jamaa wa airport wakanipigia wakaniambia kuwa Kuna mzigo wangu wameupokea kutokea uingereza na umeshalipiwa Kila kitu ni Mimi kwenda na kitambulisho Changu tu nikauchukue. Nikawaambia Mimi sipo Kenya nipo Tanzania Kama wanaweza kuutuma wautume. Kwa sehemu niliyowaambia wakasema inagharimu shilingi 125,000 ili mzigo ufike uwanja wa ndege niliopo.wamenionesha na picha ya mzigo kabisa ndio ule uliotumwa Kule uingereza. Sasa najiuliza hii kitu imekaaje? Maana wao wanasema mzungu kalipia mzigo mpaka pale ulipofikia Ila hizo gharama za kuja huku Tanzania ni gharama nyingine kwakuwa mzigo unatakiwa kukatiwa ticket na hiyo ni gharama ya ticket. Na njia ya malipo wamesema naweza kutumia mpesa au Tigo pesa. Ndo najiuliza hapa nitumie au nakaribia kutapeliwa? Maana Sina uzoefu na upokeaji wa mizigo iliyotumwa kutokea nje ya nchi. Nawasilisha wakuu. Naombeni ushauri wenu
Kimbia mbio unapigwa ww.

Hakuna cha mzungu wala nini kuna wajinga tu wapo hapa mjini wanakuchezea mchezo.
 
Sema tu sijawahi kutukana mtu hapa JF vinginevyo leo haki ya nani ningekuporomoshea matusi non stop kmmk. Basi tu! 😬😬😬🚮

cutenither_20210529_205148_4.jpg
 
Kisa Changu Kiko hivi, Kuna mzungu aliniomba urafiki Facebook baada ya kumkubalia akaniomba namba ya Whatsapp. Tukaanza kuwasiliana ndani ya siku mbili tatu akaahidi kunitumia mzigo ambao ni simu ya iPhone 16. Yeye anaishi London uingereza na siku aliyotuma mzigo alisema kuwa amekosa ndege inayokuja moja kwa moja Tanzania hivyo akatuma kwenye ndege inayoishia Kenya maana walimwambia kuwa mzigo ukifika wanaweza kufanya delivery uwanja wa ndege ulio karibu (hapahapa East Africa). Basi bwana yule mzungu akatuma mzigo na akanitumia picha ya mzigo pamoja na risiti na zote Zina majina yangu maana aliniambia nimtumie majina yote matatu na namba ya simu, na akaniambia mzigo utafika Nairobi baada ya masaa 9 na akanisisitiza kuwa niwe Makini na muda kwani mzigo ukishafika watanijulisha na kweli baada ya masaa Tisa (mzigo aliutuma saa 2 usiku saa 11 ukawa umefika Jomo Kenyatta Airport Kenya)
Wale jamaa wa airport wakanipigia wakaniambia kuwa Kuna mzigo wangu wameupokea kutokea uingereza na umeshalipiwa Kila kitu ni Mimi kwenda na kitambulisho Changu tu nikauchukue. Nikawaambia Mimi sipo Kenya nipo Tanzania Kama wanaweza kuutuma wautume. Kwa sehemu niliyowaambia wakasema inagharimu shilingi 125,000 ili mzigo ufike uwanja wa ndege niliopo.wamenionesha na picha ya mzigo kabisa ndio ule uliotumwa Kule uingereza. Sasa najiuliza hii kitu imekaaje? Maana wao wanasema mzungu kalipia mzigo mpaka pale ulipofikia Ila hizo gharama za kuja huku Tanzania ni gharama nyingine kwakuwa mzigo unatakiwa kukatiwa ticket na hiyo ni gharama ya ticket. Na njia ya malipo wamesema naweza kutumia mpesa au Tigo pesa. Ndo najiuliza hapa nitumie au nakaribia kutapeliwa? Maana Sina uzoefu na upokeaji wa mizigo iliyotumwa kutokea nje ya nchi. Nawasilisha wakuu. Naombeni ushauri wenu
Wanakuibia hao sasa hivi mkuu, hiki kisa chako kinafanana na yule jamaa anaejiita Side Mzee wa kushenyenta niliwahi kumskia pahala akihadithia tukio kama hili na mwisho wa siku walimuibia.

Pia kuna ile njia ya check ambayo hii Mimi ni shuhuda mzuri sana kwa maana kwa njia hii nilipigwa kizembe sana na yule kuku mwekundu 😅😅😅.
 
Back
Top Bottom