Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Watanzania wenzangu wenye kupende maendeleo ya nchi yetu naomba mtujuze ni utaratibu gani halali unatakiwa kutumika kikatiba na kisheria kumuondoa raisi madarakani.Sisi ndio waajiri wake ila ikifika hatua baadhi yetu haturidhiki na utendaji wake tunatakiwa tutafute njia halali za kisheria kumuondoa kwenye nafasi yake badala ya kila siku kuwa walalamikaji tu bila kuchukua hatua.
Mimi huwa najiuliza hivi inakuwaje karibu nchi nzima kuanzia wanaharakati,wanasiasa,waandishi wa habari,makundi mbali mbali ya kijamii na watanzania wengi wakilalamika kutaka watu fulani, ambao wengi wao huwa ni wateule wa raisi, wachukuliwe hatua halafu hakuna kinachofanyika.Na hata pale hatua zinapochukuliwa basi huwa ni baada ya watu kulalamika na kupaza sauti sana.Sasa huyu mheshimiwa yeye huwa dhamira yake haimsukumi kuchukua hatua au yeye huwa haoni uchungu kama watanzania wengine?Uzalendo wa viongozi wetu uko wapi siku hizi?
Ni jambo la kushangaza na kuhuzunisha kuona mpaka sasa IGP,na RPC wa Iringa bado wapo ofisini.Hawa ni watu ambao wakati uchunguzi unaendelea walipaswa kuwa teyari wameshajiuzulu au kuondolewa ktk nafasi zao.Hivi ule ushahidi wa picha hautoshi kuthibitisha ushiriki wa polisi katika unyama ule?Sasa hawa wakuu wao wa kazi mbona mpaka leo wapo ofisini na ukizingatia hizi tuhuma za polisi kuua raia ni jambo la mara kwa mara.
Hali hiyo ya kulindana ilikuwa hivyo hivyo baada ya taarifa ya CAG kuonyesha uozo serikalini.Ilibidi kelele zipigwe ndio hatua zikachukuliwa.Sasa kwa mwendo huu tutafika salama hiyo 2015?Tuna haja kweli ya kusubiri mpaka muda huo ufike?
Hivi leo hii nani anajua nini kinaendelea kuhusu Jairo,watuhumiwa wa richmond,kagoda,meremeta na wengine wengi tu.
Swali langu ni kwanini sisi tuwe watu wa kulalamika tu bila ya kuchukua hatua za kinidhamu kama ambavyo yeye hutishia kuwachukuli hatua walimu na madaktari waliogoma?Yeye kama mtumishi wa umma si anapaswa kuwajibika kama watumishi wengine?
Wanasheria aanzisheni mchakato wa kikatiba na kisheria na sisi tutawaunga mkono.Tusisubiri bunge limuwajibishe kwani lile bunge liko kichama zaidi.Vinginevyo tutendelea kulalamika mpaka 2015.
Nawasilisha.