Ni utoto wa hali ya juu kuamini Kama Kuna watu wanazuia mvua kunyesha

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Aisee Kuna watu sijui niseme Ni elimu ndogo au Ni imani tu potofu kukithiri akilini eti mtu anakusimulia visa vya kichawi kwamba Kuna watu Wana uwezo wa kuzuia mvua kunyesha.jamani elimikeni nyie ambao bado mnaendelea kuamini dhana ya uwepo wa uchawi kifupi hakuna kiumbe chochote ambacho kina weza kuingilia nature ya ulimwengu na kikafanya mchezo kuchezea hydrologic cycle.sio mchina,sio msukuma sio mkigoma,sio msumbawanga hakuna yoyote mwenye uwezo huo.hakuna uchawi wa kutengeneza radi hizo Ni stories tu ambazo hakuna shahidi isipokuwa nyote mmezisikia kwenye masimulizi.hakuna uchawi wowote fikirini nje ya box bndugu zangu kifupi uchawi au ushirikina Ni ile Hali ya mtu kujitenga na Mungu,so mtu anapokuwa mbali na Mungu means Hana subira atakuwa akimaini Jambo lake lingine lakini Hilo Jambo halijawahi kumletea matokeo anayotaka ila yeye ataendelea TU kuliamin.huo ndo uchawi yaani yeye anakuwa akiamini kwamba Kuna matokeo fulani yatatokea akivunja Nazi barabarani lakini hakuna linalotokea lenye uhusiano na alichokifanya.. practically inafanywa lakini outcome hakuna.ni Kama dhambi TU ukiianza utakuwa mtaalam wa dhambi hio kiasi kwamba utabuni mpaka njia mpya za kuiboresha dhambi yako na kuiacha inakuwa Ni ngumu,so na mchawi ndo hivo hivo.
au mfano rahisi Ni kama kubet unaamini utashinda lakini hushindi na siku ikitokea ukishinda unaamini inawezekana.so hata uchawi mtu anadanganywa na mganga amuloge fulani aumwe so huyo fulani hata akiumwa ugonjwa wa kawaida Kama kansa au kisukari nyie mtaamini uchawi ndo umewawezesha kufanya aumwe..hio ndo reality iliyopo na ndo maana hata hao ambao mnaamini Ni wachawi wanakufa na kuumwa kama sisi na wanakuwa na matatizo Kama yetu tu mawazo Kama yetu stress Kama zetu,umaskini Kama Sisi wakati sote tunajua hakuna asiyependa shida hapa duniani sote tunapozaliwa tunajitahidi kutafuta mafanikio ambayo yataonekana kwa watu na kutupa faraja lakini hao wachawi hakuna wanalopata ndo kwanza Wana maisha magumu.wanatamani Wapate wepesi lakini hawapati so kwa kuwa hawamtegemei Mungu wanaendelea kusumbuka na ulozi na kwa ujinga wao Mungu anawapiga pigo na kuwaachia waendelee kuhangaika kuamini ipo siku Miungu Yao ya sanamu itajibu lakini haijibu ipo kimya na maisha yanaendelea hivihivi chini ya jua.miliki ya Mungu inaendelea kujengwa kwa kutumia nguvu na sio maajabu..hakuna uchawi msiogope Mambo ambayo hayapatani na akili.

Uongo na ukweli tofauti yake Ni inch 2.5 - JamiiForums
 
Nilishawahi kwenda kwa mganga ili kumfanya bebee wangu asipende hela lakini ikashindikana

Toka hapo siamnini waganga!
 
Mtoa mada utakua ni mwanaume wa dar, hujatembea mkoani na wala hujakutana na wale wanaofanya biashara ya tofali za kuchoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wabaya wa huyo Mungu ni vitu gani!?.. Unajua lakini kinyume cha mwanamume ni mwanamke?.. je kinyume cha Mungu ni nini?..
Kwamba Mungu anaweza hamisha mlima kilimanjaro lakini mchawi hawezi pita ukutani!. Yani unaamini Mungu yupo, huamini uchawi kuwepo!?..
kinyume cha dada ni kaka, baba ni mama, Uchawi ni Uungu!.
Huamini mchawi kuzuia mvua, utatuaminisha vipi Mungu huleta baraka!?..
 
Don't compare supreme power with chemistry.
 
Kinyume Cha Mungu(ukweli) Ni ujinga(uongo) na sio uchawi.
 
-The Chinese recognize the value of weather modification and believe that the US military continues to use weather as a weapon.

-Many countries throughout the world practice weather modification. The Russians have long
been interested in using weather modification as a way to control hail.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…