Ni uwezekano wa kiasi gani kupata maambukizi ya h.i.v??msaada please

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
16,950
Reaction score
13,527
Salaam,

Kuna ndug yangu kanipatia swali ambalo kwa kweli mimi sina elimu nalo ya kutosha,mwenye ujuzi anisaidie nipate cha kumjibu..

"AMEKUTANA KIMWILI "KAZINI","KASEX","KAFANYA TENDO LA NDOA" N,K na binti wa makamo yake,umri wa miaka 32 kama yeye,ila hawana mahusiaono rasmi ya kindoa,

Yapata miaka mitatu alikuwa nje ya nchi kimasomo,kipindi anasoma mahusiano yake na mchumba wake yalikuwa ni kwa njia ya mawasiliano tuh na walifanikisha kujenga mahusiano yao,

Alipomaliza masomo mwaka huu nakurud nyumban TZ aliendeleza mahusiano yake kingono na mwenza wake,

Juzi anasema hakutumia KINGA kwa tendo hilo,anasema japo alienda mshindo mara moja tuh,alimwandaa vyema mwenzake na pia hakuwa na michubuko katika maungo yake ya siri,kinachompa stress ni kwamba haijui afya ya mwenzake kwani hawakupima hivi alivyorudi kutoka masomoni,,

Tujaalie yule mwenzake ana H.I.V,vipi uwezekano wa yeye kuupata ugonjwa huo ukoje??

Kama alimuandaa vyema mwenzake na kusex nae kwa mshindo mmoja wa dakik kadhaa,tuseme si chini ya kumi,asilimia yake yeye kupata maambukiz zikoje//

Ahsante Natanguliza..
 
Subiri week 4 hv uende ukacheki..
But nina mashaka mkuu sio wewe kweli?
 
Mwambie aachane na mambo ya takwimu.Kaka amepata kapata na kama hajapata basi amshururu mungu wake.Kanuni ya takwimu ni kwamba hata kama chance inakuwa ndogo kiasi gani,inawezekana ikawa ndiye yaliyepata chance hiyo!

Hata kama utaambiwa ni 15% au 1.5% haina mantiki yoyote.Maana inawezakuwa ni miongoni mwa hao watu 15 katika mia au 15 katika elfu moja,who knows?! Hapo cha kufanya yeye atulie tu kama imetokea imeishatokea,kikubwa angaalie mbele na aendelee na maisha yake kama kawaida.Utakapofika muda muafaka akapime awe na uhakika.

Mimi huwa nawashangaa sana watu wa ina hii,kwani wale watu wanaoishi na VVU wao sio watu?Mnafikiri wao hawana damu?Mbona tunao watu wengi tena wengine ni maarufu na tunawatetemekea kila siku,lakini wanaishi na VVU?! Au kwa vile hatujui status zao?Ikitokea mtu ameambukizwa VVU bado maisha yataendelea.

Wewe mwambie huyo jamaa yako atulie tu,maana hata akipanic haitasaidia kitu.Yeye ajichukulie ni aidha ameambukizwa au hajaambukizwa.Muulize,ikiwa hajaambukizwa,je ana hakika hataupata huo ugonjwa maishani mwake tena?Nonsense.Haya ni maisha na ni lazima yasonge.Mwambie kuna mengi tu yatafuata.Leo anakuja na hili,hatujui kesha au mwakani atakuja na lipi.Mwambie aconcetrate na shughuli zake,asije kujikuta amepoteza muda wake mwingi akapoteza hata alichonacho,halafu mwisho wa siku akapimwa akakutwa hana tatizo.
 
kijana nikupe wazo wa kufanya maamuzi magumu,,,,,
Ukimwi upo na unaua
Maralia ipo na inaua,,,
Kisukari kipo na kinaua,,
Saratani ipo na inaua

Ukiamua kupima ukimwi pima,,
Ila tambua kuna majibu mawili tu! Unao au hauna,,
Je ukikutwa unao utafanyaje?
Je ukiwa hauna utafanyaje pia?
Ndio maana wanasema kupima ni hiari ya mtu hawalazimishi.
 
Ili mtu apate UKIMWI ni lazima michubuko iwepo ili kuruhusu majimaji kupenya.Ila mwambie asito*** hovyo dunia imehrbk
 
Kwanini aishi kwa wasiwasi kama ni mpenzi wake kweli si aende akapime tu yaani amshawishi. Hapa nachoona ni kuwa huyu si mpenzi wake ila tu ni demu wa kupita. Unalo hilo mwanawane.
Lakini hata ukijua % hazikusaidii coz utakuwa huru baada ya miezi 3 ukipima. Any way
insertive ni 0.03 - 0.09% yaani kwa male, kwa female receptive 0.3 - 0.9%. Kama hayajapita masaa 72 nenda angaza wakupe PEP yaani post exposure prophylaxis. All the best
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…