Ni uzalishaji gani rahisi?

klorokwine

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
378
Reaction score
31
Wakuu naomba kupata mawazo yenu juu ya bidhaa gani naweza kuprocess na kuzalisha hapa nchini,
Hasa ukizingatia nahitaji kutumia mashine rahisi na mtaji kidogo (usiozidi tsh mil 5)
Muhimu kuzingatia upatikanaji rahisi wa mali ghafi za hapa hapa nyumbani.
Naomba mchango wenu wadau.
 
Kwa swali lako ni sawasawa na unaomba watu wakupe Business Idea zao kitu ambacho Kwa mimi nahisi ni kigumu na itakuchukua muda kukipata.

Cha msingi kaa chini angalia mazingira yako yanayokuzunguka na tafuta opportunity ya kitu gani kina-miss then fanya production ya hicho kitu....!

Kila la heri Mkuu!
 

Aisee kumbe unajua kutoa nondo kwa Wenzi Kizzy.

Mbaya zaidi mleta ni kwamba hajafahamika hasa anataka nini,ni mbaya sana.

Kijana lazima kwanza uwe na plans kichwani then ufanye utafiti kisha uulize ili upewe mbinu.
Lakini la sivyo unaweza kufanya biashara kwa kufuata mkumbo mwisho wa siku ukadunda
 

Hahaa,
Mkuu halafu nimeshindwa kuliona hilo jukwaa la wajasiriamali ulilonielekeza!
Sijui utaweza kunielekeza kama hutojali?
 
Hahaa,
Mkuu halafu nimeshindwa kuliona hilo jukwaa la wajasiriamali ulilonielekeza!
Sijui utaweza kunielekeza kama hutojali?

Kamanda nenda kwenye Page hapo juu kabisa imeandikwa home.
Click hapo,then kutakuja Bars kadhaa,shuka chini kuna sehem imeandikwa GENERAL FORUM kisha shuka chini utakuta Link kibao,then ukiendelea kusha utakuta link imeandika Ujasiriamali.
Kwa kuanzia nimekuwekea hapa ili usipate tabu ,click link hii hapo chini
Ujasiriamali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…