gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,312
- 3,345
Hii ni mada nzuri kuijadili kwa pamoja japo mimi nitatoa tafsiri yangu.Nimevutwa na hili kutokana na mazingira magumu ya sasa,wapo wengi wanamwomba Mungu lakini mahitaji yao hayatimii,wapo wanaosumbuliwa na mapepo lakini wanapoombewa hawaponi,kwanini?
Ili kuelewa kwa urahisi kabisa hemu chukua mfano huu rahisi wa mtu anaefanya mazoezi yakupiga push up.
Mtu anayepiga push up hamsini kama mazoezi,basi zoezi lenyewe huwenda likawa zile pushup 10 za mwisho kabisa.Hapa namaanisha 40-50 zitakuwa push za taabu na huwenda ile push up ya 50 akaishia nusu kwa uchovu.
Huwezi kusema umefanya mazoezi wakati umepiga pusbup moja.
Sala ni ile hali ya utulivu wa juu kabisa kwa mwanadamu ili kuongea na Mungu wake kwa tafakari ya juu kabisa.Vinginevyo kama mtu ataomba Sala yoyote ile pasipo hilo basi huyo hawezi kupata hitaji lake.
Mungu hatuongei naye kwa sauti bali tafakari ya kina na hapa ndipo kwenye msingi wa imani.