philosophy
Senior Member
- Nov 11, 2012
- 104
- 42
NI VIATU VISIVYO VYETU.
Kale ilipokuwa,
Viatu tulivijua,
Vilitupendeza,
Mguuni tulivaa.
Tulivivaa vikavalika,
Hakika tulifurahia,
Kila aliye, alikabiri,
Viatu vilikuwa sawia.
Mambo yageuka,
Viatu twavua,
Vya kwetu nuksi,
Vya wale twavaa,
Akili yatwaliwa.
Muda ukienda,
Mambo hubadilika,
Akili huchanganya,
Hata kutofikiri pia,
Viatu hivi havitufai.
Hatuioni, iliyo yetu,
Vya wale ndio rasmi,
Vya kwetu si lolote,
Wakati vimepitwa,
Viatu hivi havitufai.
Wingi wa viumbe,
Nalo ndo zao,
Haiajalishi ni nani,
Almradi wengi wape,
Viatu hivi havitufai.
Hakuna utofauti,
Ujinsiya usiwepo,
Japo tupo ki kaida,
Kelele zitapigwa,
Pasi na kutafakari.
Sera utazikubali,
Za kwenu si mantiki,
Utaonekana hufai,
Mpaka utambuliwe,
Kwa nini usijijue?
Jinsia moja uhusiano,
Haki mwenye kutaka,
Urazini umeamua,
Wachache waitikia,
Kinywa chanena.
Maisha twayaishi,
Si yetu twaghairi,
Uhuru uko wapi?
Viatu hivi si vyetu.
Sambamba na wakati,
Sie twajitamba,
Kinyume chake kipo,
Viatu hivi si vyetu.
Vijana hawajitambui,
Viatu hivi kisababishi,
Mwelekeo wapotea,
Viatu hivi si vyetu.
Ya kale si dhahabu tena,
Masikioni ni -----,
Ukiyanena utatengwa,
Mshamba utaitwa,
Adhaze ndo mtoto,
Dhoruba yashika atamu,
Lawama twajitupia,
Tulipuuza pasi kujua,
Matokea ni haya,
Viatu hivi havitufai,
Turudie vyetu!
Kale ilipokuwa,
Viatu tulivijua,
Vilitupendeza,
Mguuni tulivaa.
Tulivivaa vikavalika,
Hakika tulifurahia,
Kila aliye, alikabiri,
Viatu vilikuwa sawia.
Mambo yageuka,
Viatu twavua,
Vya kwetu nuksi,
Vya wale twavaa,
Akili yatwaliwa.
Muda ukienda,
Mambo hubadilika,
Akili huchanganya,
Hata kutofikiri pia,
Viatu hivi havitufai.
Hatuioni, iliyo yetu,
Vya wale ndio rasmi,
Vya kwetu si lolote,
Wakati vimepitwa,
Viatu hivi havitufai.
Wingi wa viumbe,
Nalo ndo zao,
Haiajalishi ni nani,
Almradi wengi wape,
Viatu hivi havitufai.
Hakuna utofauti,
Ujinsiya usiwepo,
Japo tupo ki kaida,
Kelele zitapigwa,
Pasi na kutafakari.
Sera utazikubali,
Za kwenu si mantiki,
Utaonekana hufai,
Mpaka utambuliwe,
Kwa nini usijijue?
Jinsia moja uhusiano,
Haki mwenye kutaka,
Urazini umeamua,
Wachache waitikia,
Kinywa chanena.
Maisha twayaishi,
Si yetu twaghairi,
Uhuru uko wapi?
Viatu hivi si vyetu.
Sambamba na wakati,
Sie twajitamba,
Kinyume chake kipo,
Viatu hivi si vyetu.
Vijana hawajitambui,
Viatu hivi kisababishi,
Mwelekeo wapotea,
Viatu hivi si vyetu.
Ya kale si dhahabu tena,
Masikioni ni -----,
Ukiyanena utatengwa,
Mshamba utaitwa,
Adhaze ndo mtoto,
Dhoruba yashika atamu,
Lawama twajitupia,
Tulipuuza pasi kujua,
Matokea ni haya,
Viatu hivi havitufai,
Turudie vyetu!