Ni vigezo gani huzingatiwa kupromote Dokta kuwa Profesa nje ya Academia

NJOGHOMILE

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2017
Posts
694
Reaction score
1,942
Nimezoea kuona watu kwenye field ya Academia wakiwa wanapata promotion ya kutoka Udokta na kuwa Associate Professor ambapo baadae atakuwa Full Professor.

Vigezo ambavyo nimezoea kuviona vikizingatiwa katika hizo promotion ni Teaching Points, Publication kwenye peer review journals na Book Chapter. Pia mamlaka zinazohusika kupromote huwa ni hizo hizo Academia anapopractise huyo mtu.

Je, kwa mtu ambaye yupo nje ya Academia, ni vigezo gani huwa vinazingatiwa ili mtu kuwa promoted kutoka Dokta na kuwa Associate Professor /Full Professor. Pia ni mamlaka zipi zinahusika katika hizo promotion za watu walio nje ya Academia.

Mfano aliyekuwa Katibu Mtendaji wa NECTA kuanzia enzi za awamu ya 5 alikuwa ni Dokta ila sasa ni Professor. Huwa najiuliza kila mara nashindwa kupata jibu.

Nina imani hapa nitapata majibu kuhusu hili jambo
 
Swali nzuri.

Huyo Katibu Mkuu ni nani?

Kama ni Ndalichako alipotoka Necta alirudi UDSM hapo hapo
ndio alipopatia uprof wake.

Pia wengine ambao wana majukumu mengine huwa wanafanya
part time teaching na kusimamia research huko vyuoni ndio baadae
wapanda ngazi.
 
Ndio yeye mkuu, kumbe alirudi UDSM

Nakumbuka hadi mwaka 2015, alikuwa NECTA, mwaka 2016 ndipo aliteuliwa kuwa mbunge na Kupewa Uwaziri wa Elimu. Sasa mbona inaonesha muda aliorudi UDSM ni mdogo sana kiasi kwamba kuja kupata hizo point za Promotion sio rahisi.

Au waliangalia uzoefu wake NECTA?

Mfano Prof Hosea, sio ndio
 
Alijuzulu NECTA kipindi cha Kikwete mwishoni akaenda UDSM sasa huwezi jua kama

alikuwa akifanya part time UDSM tangu yupo NECTA kwa sababu mwanzo kabla ya
NECTA alikuwa huko UDSM.

Yes kama Prof Hosea na wengine wanaofanya hivyo.
 
So kama una undergraduate GPA 3.8 na Master GPA 4 na PhD tafuta hata

vyuo vya Private ufundishe part time utapanda kufikia level hiyo ya Uprof.
 
Inategemea na sehemu.

Marekani Professor ni mwalimu wa chuo kikuu tu.

Kuna jamaa mmoja alikuwa anafundisha chuo kikuu Marekani tukawa tunamuita doctor, akasema msiniite doctor kwa sababu sijamalizia PhD yangu, niiteni Professor.

Kwa hiyo Marekani inawezekana mwalimu wa chuo kikuu ambaye hana PhD akaitwa Professor. Na mwenye PhD ambaye hafundishi chuo kikuu asiwe Professor ila akawa doctor.
 
Kwa hiyo Marekani inawezekana mwalimu wa chuo kikuu ambaye hana PhD akaitqa Professor. Na mwenye PhD ambaye hafundishi chuo kikuu asiwe Professor ila akawa doctor.
Sawa sawa utofauti huo. Basi PhD ndio mwisho wa vyote.
 
Alijuzulu NECTA kipindi cha Kikwete mwishoni akaenda UDSM sasa huwezi jua kama

alikuwa akifanya part time UDSM tangu yupo NECTA kwa sababu mwanzo kabla ya
NECTA alikuwa huko UDSM.

Yes kama Prof Hosea na wengine wanaofanya hivyo.
Kumbe lile sekeseke la kutakiwa kujiuzulu sababu ya matokeo ya Dini kuvurugwa lilimpelekea kuwajibika

Kama kweli aliendelea kufanya part time, hapo sawa
 
Inategemea na sehemu.

Marekani Professor ni mwalimu wa chuo kikuu tu.

Kuna jamaa mmoja alikuwa anafundisha chuo kikuu Marekani tukawa tunamuita doctor, akasema msiniite doctor kwa sababu sijamalizia PhD yangu, niiteni Professor.

Kwa hiyo Marekani inawezekana mwalimu wa chuo kikuu ambaye hana PhD akaitwa Professor. Na mwenye PhD ambaye hafundishi chuo kikuu asiwe Professor ila akawa doctor.
Wenzetu wanajua thamani ya Mwalimu, kuitwa Professor ukiwa Mwalimu, inastahili
 
Watanzania wengi wana Status Anxiety.

Mfano watu wengi wanataka title, Dr., Professor, Engineer, CPA, etc. Hata sehemu ambayo title haihusiki.

Huku kwingine unaweza kumsikia mtu anaitwa "Robert Gates, Secretary of Defense" kika siku. Ukienda kuangakia profile yake unakuta kumbe jamaa ana PhD lakini husikii watu kumshobokea kumuita Dr. Gates. Mpaka labda umkute kwenye settings za academia.

Sisi Dr. Samia, Dr. Kikwete, mpaka kuna siku watapewa wagonjwa watibu.
 
Uprofessor ni lazima kutoka katika chuo. Yaani professor huyo awe anajishughulisha na shughuli za msingi za chuo yaani kufundisha au na tafiti. (Teaching and or research)
Na watu wanaoitwa Dr Fulani ni walio hitimu Phd na aidha ni waalimu wa chuo au matabibu hospitalini. Wengine haifai kutumia title ya Dr
 
Watanzania wengi wana Status Anxiety.

Mfano watu wengi wanataka title, Dr., Professor, Engineer, CPA, etc. Hata sehemu ambayo title haihusiki.

Huku kwingine unaweza kumsikia mtu anaitwa "Robert Gates, Secretary of Defense" kika siku. Ukienda kuangakia profile yake unakuta kumbe jamaa ana PhD lakini husikii watu kumshobokea kumuita Dr. Gates. Mpaka labda umkute kwenye settings za academia.

Sisi Dr. Samia, Dr. Kikwete, mpaka kuna siku watapewa wagonjwa watibu.
Hahahah mkuu ni pombe gani hiyo inayokupa hasira hivyo.
 
Swali nzuri.

Huyo Katibu Mkuu ni nani?

Kama ni Ndalichako alipotoka Necta alirudi UDSM hapo hapo
ndio alipopatia uprof wake.

Pia wengine ambao wana majukumu mengine huwa wanafanya
part time teaching na kusimamia research huko vyuoni ndio baadae
wapanda ngazi.
Dah ndalichako na ile English anafundishaje?
 
Hahahah mkuu ni pombe gani hiyo inayokupa hasira hivyo.
Nina zaidi ya mwaka sijanywa pombe ya aina yoyote.

Mara ya mwisho nilikunywa pombe ilikuwa Champagne ya kusheherekea mwaka mpya wa 2024, January 1 2024.

Juzi January 1 2025 ilikuwa mwaka mzima tangu nimekunywa pombe ya aina yoyote.

Tatizo mnyama mkubwa hata akipiga chafya kwa reflex action tu, nzi akiwa karibu ataona mkubwa amekasirika.
 
Back
Top Bottom