Ni vigumu kulipa kodi halali labda unataka kufilisika

Ni vigumu kulipa kodi halali labda unataka kufilisika

Biok

Member
Joined
Jan 17, 2023
Posts
69
Reaction score
147
Kwa mfanyabiashara mdogo na mkubwa kulipa Kodi Halali ni vigumu sana,akilipa Kodi Halali ajiandae kufunga biashara yake (kufirisika) viwango vya Kodi ni vikubwa mno.

Wafanyabiashara wengi wanaamua kutumia mbinu kama kusema uongo juu ya mauzo ya Kila siku Ili akadiriwe Kodi kidogo,kufoji taarifa za uongo, kundika bei ndogo kwenye risiti za efd machine, kutokutoa risiti kabisa,kuingiza bidhaa Kwa njia za magendo n.k.

Mathlani unanunua mfuko wa sukari kilo 50 Kwa 130000 Kisha unauuza mfuko Kwa 135000, sasa ukiandika bei halisi hapo jamaa watakulamba mpaka mtaji, huna budi kuandika bei ya chini zaidi au usitoe risiti kabisa.

Pia Kuna Kodi plus ushuru kama usafi, ulinzi n.k, ndio maana hata jamaa wa kariakoo wamegoma kwani TRA wanataka Kodi yote ilipwe ipasavyo kitu ambacho ni kigumu kufanyika, kwa anayefanya biashara yoyote atakubaliana nami kuwa ukipeleka taarifa sahihi TRA jiandae kufirisika kwani viwango vya Kodi vilivyopo Si rafiki Kwa mfanyabiashara mkubwa na hata mdogo.

Mm nimeshudia mtu mwenye wastani wa mauzo ya mil 5 kwa siku anadanganya TRA kuwa wastani wa mauzo Kwa siku ni 50000,anaogopa kusema ukweli kwani atafirisika.

Nafikiri waliopanga viwango vya Kodi hawana uelewa wote kuhusu biashara na changamoto zake,hawajui faida na hasara zinazopatikana,gharama za uendeshaji,wao waliangalia upande mmoja tu wa kuongeza mapato ya serikali lkn hawajui kuwa Kodi kubwa inaua biashara pia.

Mgomo wa kariakoo uendelee labda serikali itapunguza kodi kandamizi Kwa wafanyabiashara.
 
Utitiri wa kodi na tozo na ukubwa wa hizo kodi na tozo ni janga kwa wafanyabiashara!
 
Utitiri wa kodi na tozo na ukubwa wa hizo kodi na tozo ni janga kwa wafanyabiashara!
Na huu ndo ukwel. Kodi zetu zinaua Biashara. Ebu chukulia huu mfano halisi. Kontena la foot 40 la vitenge Toka china dar linalopiwa Kodi Zaid ya ml 200 Hilo Hilo Mombasa linalopiwa ml 40 Kigali . Zambia ml 35. Yaan huku kwetu unatokaje Sasa hapo

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Hali iko hivyo kwa maslahi ya watawala na maafisa wa kodi. Hawataki kuweka kodi zinazolipika kwa sababu itawaondolea fursa zao za rushwa na kuuza ushawishi wao.
 
Nchi hii kuwa mfanyabiashara mzawa ni changamoto,wageni tu ndo wanaogopwa na utasikia wamesamehewa,mara wamepewa muda wa matazamio,Kwa mzawa vitu hivyo sahau,ndio maana wageni wanatajirika SS daily ukuaji wa mitaji yetu ni hafifu,utasikia wageni tunawasamehe Kwasababu wanatoa ajira,kwani mzawa hawezi kuajiri?kuwa mfanyabiashara nchi hii unakuwa kama mkimbizi
 
Hivi chuo Cha Kodi wanaenda kusomea ujinga?

Binafsi sijawahi kuona umuhimu wa wanachokifundisha maana Kodi nyingi zinafika mpka kwenye mtaji
 
Back
Top Bottom