Kuna watu waliweka post wakasema wanasaidia watu kusajili makampuni na kupata leseni ya biashara.Niliwaambia wao ndio wanachochea rushwa kwani taratibu za kupata vitu hivyo ziko wazi lakini wafanyakazi wa taasisi husika wamekuwa wanazungusha watu makusudi ili wapewe chochote.baada ya kuwaambia hivyo wakanishambulia wakasema wao ni wajasiria mali kwani watu wengine wako busy hawana muda wa kufatilia tratibu hizo,lakini kama kweli mtu yuko busy hwezi kufatilia taratibu hizo je ataweza kusimamia biashara aliyoanzisha kwani hiyo biashara ndio inahitaji usimamizi wa karibu ukichukulia amewekeza pesa kwa kifupi wametengeneza mtandao wa rushwa na si ajabu hata hyo mkampuni ya kusaidi kusajili ni ya kwao ila wanatumia watu wengine.
Tujifunze kwa Rwanda ambako zoezi zima linachukua dkk 45