Hapa kuna thamani real na relative.Kuna kulinganisha na vipimo kama uwezo wa manunuzi au vipimo kama dola.
Thamani ya fedha inaweza kupanda katika vipimo halisi na vipimo vya uwiano.Kwa mfano hata kama thamani ya shilingi haijapanda kwa misingi ya uzalishaji na biashara iliyotajwa hapo juu, inaweza kupanda ikilinganishwa na dola kama dola itashuka (i.e shilingi ikisimama na dola ikashuka basi shilingi itapanda ikilinganishwa na dola) au hata kama uchumi ukishuka na kusababisha nguvu ya shilingi kushuka kwa asilimia chache, lakini nguvu ya ununuzi ya dola kupungua kwa silimia nyingi zaidi, basi kwa ujumla thamani ya shilingi itapanda ikilinganishwa na dola ingawaje kiuchumi uwezo wa kununua unaweza kushuka.