Ni Vitabu vya aina gani vinavyosomwa na Watanzania na Kuandikwa na Watanzania?

Ni Vitabu vya aina gani vinavyosomwa na Watanzania na Kuandikwa na Watanzania?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu;

Kuna mtu ameniomba ushauri kwamba anataka kuwa mwandishi wa vitabu.Kwa kweli nilifurahi ila nilimuuliza analenga kuandika vitabu kwa ajili ya kina nani?Alisema Watanzania wa Rika Lolote lile?

Basi baada ya mjadala mrefu na mipango mingi nikasema nirudi hapa niwaulizeni ninyi wadau.Je, ni Vitabu vya aina gani vinavyoandikwa na watanzania?Je ni vitabu vya aina gani vinavyosomwa na Watanzania?

Je, kuna biashara katika usomaji wa vitabu hapa Tanzania?

Karibuni tujadili.
 
Watanzania wengi hawapendi kusoma ! Wanapenda udaku na mambo mepesi mepesi kama ya akina Konki Liquid!
 
Habari za wakati huu;

Kuna mtu ameniomba ushauri kwamba anataka kuwa mwandishi wa vitabu.Kwa kweli nilifurahi ila nilimuuliza analenga kuandika vitabu kwa ajili ya kina nani?Alisema Watanzania wa Rika Lolote lile?

Basi baada ya mjadala mrefu na mipango mingi nikasema nirudi hapa niwaulizeni ninyi wadau.Je, ni Vitabu vya aina gani vinavyoandikwa na watanzania?Je ni vitabu vya aina gani vinavyosomwa na Watanzania?

Je, kuna biashara katika usomaji wa vitabu hapa Tanzania?

Karibuni tujadili.
Zamani sisi tulisoma sana vitabu vya watunzi wa ndani
Kisha tukasoma vya majirani
Tukasoma pia vya African writers series
Halafu tukasoma vya ulaya na marekani vya kijasusi, historia mahusiano sayansi ,ugunduzi na ugunduzi na hata siasa
 
"Je, waafrika ndivyo tulivyo?", "Nani aliyetuloga?" "Tumbo", "Chanjo ya rushwa" "Utajitiri upo kichwani mwako", "Uhuru na kazi", "Ujamaa na Kujitegemea" na vingine vingi. Angalizo kama lengo lake ni kupata wasomaji wengi, atunge riwaya pendwa. Lakini kama anataka kuwa mwaandishi na si mtunzi ni vema angaazie ukombozi wa kifikra katika nyanja zote za ustawi wa mwanadamu, kisiasa, kiuchumi, kitamaduni (imani na mazingira), na kijamii(mila na desturi). Mtakie kila jema.
 
Kusoma kitabu ni raha Sana,kwanza kinanukia,pili unatengeneza character zako mwenyewe na mji wako,sema tu Watanzania ni wavivu kusoma.
 
Back
Top Bottom