Ni vyema DNA ikawa ni kitu cha kawaida. Mwanaume hakikisha unachunguza mtoto wako

Ni vyema DNA ikawa ni kitu cha kawaida. Mwanaume hakikisha unachunguza mtoto wako

strongest

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2024
Posts
343
Reaction score
1,562
Tunaishi katika dunia iliyojaa hila na udanganyifu. Uaminifu umepotea, na sasa kitanda kinazaa haramu

Mtoto ambae anaonesha tabia zisizoeleweka binafsi namuona haramu
—si kila unayemlea ni wako, na si kila unayemwamini ana nia njema.

Leo nimepitia Facebook, nikaona jambo la kusikitisha na kutisha. Kuna group la wanawake wakishauriana jinsi ya kubambikia wanaume watoto wasiowazalia.

Wengine wanakiri waziwazi kuwa tayari wameshawabambikia watoto wanaume wasiojua lolote.

Unalea mtoto kwa mapenzi, unamuhangaikia, unamuona kama damu yako—kumbe ni mzigo uliobebeshwa kwa hila!

Sasa imagine, umejituma, umehangaika na mtoto kwa miaka, unamuwekea msingi wa maisha, halafu anapokua anageuka kuwa shoga, mwizi, teja au mtu asiye na maadili. Ulimpa kila kitu, lakini kumbe haukujua mwanzo wake

Haukujua kama kweli ni wako. Unakuwa umebeba mzigo wa maisha usioumba, mzigo uliojaa usaliti na udanganyifu.

Unakuta mtoto ametoka kwenye bloodline ya tabia mbovu mbovu directly anakuja kuharibu kizazi chako

Hii ndiyo dunia tunayoishi leo. Wanawake wanahadaiana, wanaume wanatumiwa kama ATM za malezi, na watoto wanalelewa katika misingi ya uongo. Lakini mwisho wa siku, ukweli hauwezi kufichwa milele.

Nini cha kufanya?
DNA test iwe kitu cha kawaida

Wanaume wasibebe kila kitu kwa imani pekee—hakikisha, chunguza, na usiwe mzembe kwa maisha yako.

Watu waache kuishi kwa hila na ujanja wa muda mfupi—maana kizazi cha uongo huleta mzigo wa kweli.

Na zaidi ya yote, tuwe waaminifu kwa familia, kwa watoto, na kwa jamii nzima.

Kwa sababu, kitanda kikizaa haramu, mzigo hauwi wa mtu mmoja—unakua mzigo wa kizazi kizima.

Tafakari.
 
wengi si “mke wa mtu” ila “mke wa watu”
 
Na sheria iwepo mwanamke akimsingizia mwanaume mtoto amlipe mwanaume fidia.

Ila kwanza zile changamoto za ujauzito, kumsumbua mbaba wa watu nataka hiki sitaki hiki, leo lala chini mara rudi bafuni kaoge. Siku ya kujifungua mbaba wa watu anakimbia huku na huko kama nini sijui kuhakikisha mama na mtoto wanapata mahitaji. Moyo wake unajaa furaha kapata mtoto. Anaanza sasa malezi.

Watoto wakiwa wachanga wanavyosumbua. Mbaba wa watu anakesha ni kupokezana kubembeleza mtoto na kesho inabidi aende kazini. Bado hapo mtoto hajaumwa. Mwisho wa siku kumbe mtoto sio wake. Nachukia sana watu wazinzi kwenye ndoa.
 
Na sheria iwepo mwanamke akimsingizia mwanaume mtoto amlipe mwanaume fidia.

Ila kwanza zile changamoto za ujauzito, kumsumbua mbaba wa watu nataka hiki sitaki hiki, leo lala chini mara rudi bafuni kaoge. Siku ya kujifungua mbaba wa watu anakimbia huku na huko kama nini sijui kuhakikisha mama na mtoto wanapata mahitaji. Moyo wake unajaa furaha kapata mtoto. Anaanza sasa malezi.

Watoto wakiwa wachanga wanavyosumbua. Mbaba wa watu anakesha ni kupokezana kubembeleza mtoto na kesho inabidi aende kazini. Bado hapo mtoto hajaumwa. Mwisho wa siku kumbe mtoto sio wake. Nachukia sana wanawake wazinzi kwenye ndoa.
upo sahihi manake wanawake wa siku izi wanavuka mipaka
 
Vingine vinatekelezeka vizuri tu kama hilo la fidia wasi wasi wangu ni mtoto asie na hatia kuumizwa
 
Back
Top Bottom