SoC03 Ni vyema mafundisho kama ya binadamu wa kwanza alitokana na nyani yaondolewe kwenye mitaala yetu ya elimu kwasababu yanachochea ubaguzi wa rangi

SoC03 Ni vyema mafundisho kama ya binadamu wa kwanza alitokana na nyani yaondolewe kwenye mitaala yetu ya elimu kwasababu yanachochea ubaguzi wa rangi

Stories of Change - 2023 Competition

Run final

New Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
2
Reaction score
2
NI VYEMA MAFUNDISHO KAMA YA BINADAMU WA KWANZA ALITOKANA NA NYANI YAONDOLEWE KWENYE MITAALA YETU YA ELIMU KWASABABU YANACHOCHEA UBAGUZI WA RANGI KWA WATU WEUSI

UTANGULIZI
Ubaguzi wa rangi, kwa maana fupi ni hali ya kumpagua binadamu mwenzio kwasababu ya rangi yake ya ngozi. ambapo kwa mara nyingi hali hii ya ubaguzi wa rangi, imekuwa ikitokea sana kwa upande wa watu weusi kwenye maeneo mbalimbali, huku wengi wao wakinyimwa huduma zao za msingi. Kama vile huduma za afya, huduma za usafiri na wengine kunyimwa ajira, pia wengine hata kufikia kupoteza maisha kwa kupigwa risasi, kwasababu ya ngozi zao kuwa nyeusi. hivyo basi ndani ya andiko hili, nitazingumzia vitu ambavyo nimevifanyia utafiti, kwamba kwa asilimia kubwa vimekuwa vinachangia watu weusi tubaguliwe, ambapo ningependa kuona vikifanyiwa mabadiliko.

Kwanza kabisa, Tanzania ni miongoni kati ya nchi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kwenye kupinga uwepo wa ubaguzi wowote wa rangi. Kwa kuhakikisha kwamba kunakuwa na haki sawa kwa watu wote. lakini pamoja na hayo yote, bado tumekuwa na vitu ambavyo tunavifundisha ambapo vitu hivyo kwa asilimia kubwa vinachangia watu weusi tubaguliwe.

Mfano, mafundisho tunayofundisha kwenye mitaala yetu ya elimu yanayosema kwamba sisi tulitokana na nyani hapo mwanzo, alafu ikafika kipindi tukabadilika kwa kupitia hatua mbalimbali mpaka kuwa binadamu kamili. Kwa maana nyengine fundisho hili linamaanisha kwamba sisi ni manyani tulio badilika hadi kuwa binadamu wa kawaida, kitu ambacho hakina ushahidi mpaka sasa. Lakini pia, nje ya hapo ni fundisho ambalo halina msaada wowote kwa maisha ya kila siku ya mtanzania.

Pengine fundisho hili kwa asilimia kubwa linachangia ubaguzi wa rangi kwa watu weusi. Kwasababu katika tafiti ambazo nimefanya kutokana na matukio mengi ya ubaguzi wa rangi ambayo yametokea ndani na nje ya nchi, nimegundua wengi ambao wamekuwa wakibaguliwa utakuta wamekuwa wanarushiwa kama vile ndizi, wengine wanaitwa hadharani majina kama vile manyani. ambapo tukiangalia ubaguzi huu hauna utofauti na mafundisho ya nyani ambayo tumekuwa tukifundishana kwenye mitaala yetu ya elimu hapa nchini. ni wazi kwamba mafundisho haya kwa namna moja au nyingine yamekuwa yanachochea ubaguzi wa rangi kwa watu weusi.

Lakini pia, kitu ambacho kinanishangaza ni kwamba nchi nyingi hapa afrika ikiwemo Tanzania, zimekuwa mstari wa mbele kwenye kupinga ubaguzi wa rangi. lakini ukija kwenye mafundiaho yao utakuta wanafundisha kwamba wao walikuwa ni manyani. alafu kwa upande mwengine mfano akitokea mgeni mwenye rangi tofauti na nyeusi, ambaye atapitia mitaala yetu ya elimu akaona tunafundishana kwamba sisi ni manyani, alafu baadae akija kutuita watu weusi ni manyani, utakuta watu weusi wakisema kuwa ni ubaguzi wa rangi. wakati ni kitu ambacho tunakifundisha kabisa wenyewe kwenye mitaala yetu ya elimu, sasa tunapokuwa tunafundishana kwamba sisi tulikuwa ni manyani tunafundisha ili iweje.

Ni wazi fundisho hili limekuwa kama pambo tu, yani ili mradi tuonekane labda na sisi tunamasomo mengi, alafu wengi wetu hatulikubali tumekuwa tunalikataa na kulipinga vikali kwamba ni ubaguzi wa rangi, alafu wakati huo huo tumelifanya fundisho hilo kama somo la lazima kwenye mitaala yetu ya elimu. hapa tunaona kwamba tumekuwa vigeugeu, kwasababu kwa upande mmoja tunapinga ubaguzi wa rangi. alafu upande mwengine tunakubali kujibagua wenyewe kwamba sisi ni manyani. Mfano nakumbuka mwalimu wangu aliyenifundisha hili somo aliniambia kuwa yeye ni nyani, sasa sipati picha mtu mwenye rangi tofauti na nyeusi atakapo kuja kumuita nyani utasikia ni ubaguzi wa rangi.

Unajua sizani nchi Kama za ulaya zina mafundisho Kama haya kwenye mitaala yake ya elimu ni afrika tu, kwasababu unakuta mtoto wa miaka 15 kutoka ulaya anauwezo wa kuendesha hadi ndege pekeyake, lakini mtoto wa kiafrika mwenye umri huo yupo darasa la 4 anafundishwa mafundisho yetu haya ya nyani. Sio kwamba watoto wetu hawawezi kuendesha ndege wakiwa na miaka 15, lakini ni kwasababu ya mafundisho yetu yasiyo na msingi.

Hebu jaribu kufikiria mgeni kutoka ulaya mfano akifika Tanzania anakuta sisi tupo tumekomaa na mafundisho ya nyani siatatuona hatuna akili. ndio maana unakuta mtanzania akienda ulaya mfano kuomba kazi anabaguliwa. hivyo basi kuna haja ya kufanya mabadiliko kwenye mitaala yetu ya elimu, kwa kuondoa mafundisho Kama ya nyani ambayo yamekuwa ni mizigo kwa wanafunzi wala hayana msingi wowote ambayo hata sisi wenyewe tumekuwa tunayapinga vikali.​


KWA NINI FUNDISHO HILI LA BINADAMU KUTOKANA NA NYANI LIONDOLEWE KWENYE MITAALA YETU YA ELIMU
  • Ni fundisho ambalo linachochea ubaguzi wa rangi kwa watu weusi. licha ya kwamba fundisho hili ni nadharia tu, lakini limekuwa na ushawishi mkubwa hata kwa baadhi ya watu kuanza kulichukulia kama ni kitu cha kweli, hali inayopelekea watu kuanza kubaguana.​
  • Ni fundisho ambalo mpaka sasa halina ushaidi wowote wa kisayansi. Kwasababu ukiangalia fundisho hili utagundua kuwa halina uthibitisho bado na wala katika uhalisa hakuna nyani yoyote mpaka sasa aliyebadilika na kuwa binadamu.​
  • Ni fundisho ambalo halina msaada wowote katika maisha ya kila siku ya mtanzania. yani lenyewe lipo kama pambo tu, ili mradi tuonekane labda tunamafundisho mengi kwenye mitaala yetu ya elimu. lakini katika uhalisa ni kwamba fundisho hili halina msaada wowote kwa mtanzania. Kwa mfano kwenye upande wa ajira, uchumi, teknolojia n.k​

PAMOJA NA FUNDISHO HILI LA BINADAMU KUTOKANA NA NYANI KUONDOLEWA KWENYE MITAALA YETU YA ELIMU NINI KINGINE KIFANYIKE
  • Fundisho hili lichukuliwe kama nadharia tu, na wala sio kitu halisi ambacho kimetokea au kimethibitishwa. Kwasababu watu wengi wanazani labda fundisho hili la binadamu kutokana na nyani lilikuwa ni la kweli, kitu ambacho kinasababisha kuwe na imani potofu hata kupelekea kuwe na ubaguzi mkubwa wa rangi, wakizani labda ni jambo ambalo limetokea kweli au limethibitishwa kumbe ni nadharia tu, ambayo haina ushaidi wowote mpaka sasa.​
  • Fundisho hili lifanywe kama somo la hiyari ambalo mtanzania yoyote anaweza kulisoma kwa faida yake mwenyewe. Yani pamoja na kuliondoa fundiaho hili nje ya mitaala yetu ya elimu, Kama kuna mtanzania angependa kujifunza, basi ajifunze kwa faida yake mwenyewe lakini lisiwe somo la lazima kwasababu ni nadharia tu isiyokuwa na msaada kwa mtanzania.​

HITIMISHO
Ni vyema fundisho hili la binadamu kutokana na nyani likaondolewe kwenye mitaala yetu ya elimu, kwasababu halina ushahidi wowote mpaka sasa. lakini pia, wala halina msaada wowote kwa mtanzania zaidi ya kusababisha kuwe na imani potofu na kuchochea ubaguzi wa rangi kwa watu weusi.​




.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom