SoC04 Ni vyema Wananchi waelimishwe kuhusu ubia kati ya serekali na sekta binafsi katika miradi ya maendeleo

SoC04 Ni vyema Wananchi waelimishwe kuhusu ubia kati ya serekali na sekta binafsi katika miradi ya maendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

HARUNI IDDI

Member
Joined
May 31, 2024
Posts
8
Reaction score
3
Ubia kati ya Serikali na sekta binafsi katika miradi ya maendeleo ( public private partnership), katika kuleta maendeleo ya kuichumi ni muhimu, kwa Tanzania ubia kati ya serekali na sekta binafsi unaongozwa na kanuni na sheria na sera ya ubia yani (public private partnership regulations of 2011), ( public private partnership Act of 2010 as amended in 2014-2018), ( public private partnership policy 2009). Ili jamii iwe na ulewa kuhusu maswala ya ubia ni muhimu elimu kutolewa ili kuepusha maneno na misugiano kwamba rasilmali za taifa Zina uzwa kwa sekta binafsi kitu ambacho siyo kweli.

Ubia kati sekta binafsi na serekali ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania tuitakayo katika miaka mitano ijayo nakuendelea ili kuweza kufikia maendeleo ya kuichumi na kuinua Kipato Cha wananchi;
Sekta zifuatazo Zina onyesha jinsi gani ubia kati serekali na sekta binafsi umeweza kuzaa matundaa hivyo serekali iweke mazingira mazuri zaidi ili kuvutiia ubia zaidi;

Sekta ya Nishati; Katika sekta ya Nishati kwa hapa Tanzania ubia kati ya serekali na sekta binafsi umeweza kuleta maendeleo na mabadiliko na kuchochea uchumi wa taifa, Mfano mradi wa songas gesi ambao una zalisha megawat 196 kutoka kwenye gesi asilia ambapo serekali kupitia Tanesco Ina miliki asilimia 46% na songas Ina miliki 54% ya umiliki hivyo jamii ukipata elimu zaidi itaweza kupata uelewa na kuonyesha ushirikiano kwa serekali kwenye kuingia ubia na sekta binafsi.

Sekta ya uchukuzi; Katika sekta ya uchukuzi serekali iliona Kuna haja ya kufanya kazi na sekta binafsi, Mfano ubia wa serekali na kampuni ya DP world kwenye undeshaji wa bandari serekali ilipata ugumu wa kufanya kazi na sekta binafsi kwa kuwa wananchi wana Imani potofu kuhusu ubia hivyo kuona kama rasilmali zita kuchukuliwa na sekta binafsi.

Sekta ya miundombinu; Katika sekta ya miundombinu ya barabara, reli, na usafiri wa anga Kuna haja ya sekta binafsi na serekali kufanya kazi kwa ukaribu na kuelimisha jamii faida zinazotokana na ubia, Mfano ujenzi wa daraja la kigamboni, ambapo ubia kati ya serekali na kuu na Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF), ulifanikisha ujenzi wa daraja kukamilika kwa wakati na ubora, pia ujenzi wa kituo cha mabasi morogoro msamvu ubia kati ya manispaa na shirika mfuko wa hifadhi ya jamii wa serekali za mitaa (LAPF).

Pia ujenzi wa soko la kimataifa la mwanjelwa ambapo ubia kati ya serekali na benki ya CRDB benki uliweza kufanya ujenzi kukamilika kwa ubora na kuleta maendeleo ya kuichumi kwa wananchi hivyo wananchi wana paswa kuelimishwa ili kuunga mkono juhudi za serekali kufanya kazi na sekta binafsi.

Sekta ya Afya; Kwenye sekta ya Afya pia ubia kati ya serekali na sekta binafsi umeweza kuzaa matundaa licha ya faida hizo lakini bado wananchi uelewa wao kwenye maswala ya ubia ni mdogo, Mfano ubia kati ya serekali na sekta binafsi na taasisi za kidini kumewezesha kuwepo kwa hospitali za Rufaa za kanda kama vile Kilimanjaro christian medical center (KCMC), na Bugando medical center na kuwezesha kutolewa kwa huduma Bora za Afya kwa bei nafuu zaidi.

Sekta ya fedha; Ubia kati ya serekali na sekta binafsi umeweza kuleta faida kwani taasisi nyingi za kifedha ambazo awali zilikuwa Zina milikiwa na serekali kwa asilimia 100% uwezo wake wakuhudumia na uwezo wake wakufanya kazi za ulikuwa mdogo hivyo baada ya serekali kushirikiana na sekta binafsi serakali imekuwa ikipata gawio kutokana na uwekezaji wake kwenye benki kama NMB, NBC, CRDB n.k

Sekta ya madini; Sekta hii ni miongoni mwa sekta zinazo changia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa taifa kutokana na unyeti wake mfano ubia kati ya serekali na sekta binafsi kwenye uchimbaji wa madini kama vile dhahabu, almasi, Tanzanite, kumeweza kuleta maendeleo makubwa katika taifa kutokana na ulipaji wa Kodi na urejeshaji kwa jamii, Mfano pia migodi kama Barrick noth mara gold mining, Geita gold mining (GGM) n.k

Sekta ya maji; Sekta hii pia iliiweze kufanya kazi kwa ufanisi na kukidhi haja ya mahitaji ya wananchi Kuna haja ya kufuta mwekezaji kutoka sekta binafsi ili kuleta mabadiliko yatakayo endana na mahitaji halisi ya wananchi Mfano kuanzisha mifumo ya Tehama katika kufatilia billi za maji kwa wateja.

Sekta ya michezo; Kutokana na taifa kujiandaa na michuano ya afcon 2027 serekali inapaswa kufanya kazi na sekta binafsi bega kwa bega ilikuweza kufanikisha uwepo wa mashindano hayo kwa ubora sekta kama za hoteli, viwanja vya mazoezi, usafirishaji, serekali inapaswa kufanya kazi na sekta binafsi ilikupunguza mzigo wa fedha za maandalizi kwa serekali pekee yake.

Hitimisho ubia wa serekali na sekta binafsi ni muhimu kwa maendeleo ya kuichumi katika miaka mitano ijayo nakuendelea hivyo jamii inapaswa kupewa elimu ilikuepusha mitazamo hasi juu ya ubia nakuhisi kuwa rasilimali za taifa kuchukuliwa na sekta binafsi kitu ambacho siyo kweli bali pande zote hufaidika hivyo Kuna haja ya elimu kwa umma juu ya maswala ya ubia kutolewa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom