SoC01 Ni wajibu wetu kutunza vyanzo vya maji

SoC01 Ni wajibu wetu kutunza vyanzo vya maji

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Endapo tukitunza vyema vyanzo vya maji na kuweka sheria zitakazoweza kusimamia matumizi mabaya ya vyanzo vya maji hii itatusaidia kutuepusha mbali na magonjwa na kuimarisha afya zetu pia

Ili kuishinda malaria tunatakiwa pia kulizingatia hili ambapo ni moja kati ya sababu kubwa ya mbu na bacteria kuzaliana na endapo vyanzo hivyo vitakuwa vichafu ni kwamba tutafungua milango ya magonjwa ambayo itapelekea kupunguza kasi ya maendeleo na nguvu kazi ya taifa letu hivyo tuchukue tahadhari.

Pia tukumbuke kwamba tukapo vitunza vyanzo vya maji inavyotakiwa ni kwamba tutaweza kuwanusuru viumbe wa majini kufa ovyona badala yake kuwalinda na kustawisha uoto wa asili ambao ndiyo misingi bora ya kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuondoa gesi za ukaa katika angahewa na hatimaye kuwa sehemu ya kujivunia kwa maisha yetu.

1. Hivyo tusifanye shughuli za viwanda karibu na vyanzo vya maji na pia ziwekwe sheria za utunzaji,

2. Tusikate miti karibu na vyanzo vya maji.. 3.Tutumie uvuvi wa kisasa usiyo haramu ili kuwaokoa viumbe waliopo majini ili waendelee kuzaliana zaidi na zaidi.

Sekta ya utalii ni miongoni katika sekta zinazo chochea ongezeko kubwa kwa pato la taifa letu.
Hivyo mazingira yetu kwa kuangazia uoto wa asili na vyanzo vya maji huchochea sura nzuri ya nchi yetu ambapo huwashawishi wageni mbalimbali kuja kutembelea hifadhi mbalimbali katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na kujifunza baadhi ya tamaduni kutoka kwetu.

Tujitahidi kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na uoto wa asili na wanyamapori sambamba na kukemea shughuli za ukataji miti ovyo inayopelekea athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa Kiasi kikubwa.

Pia usimamizi mzuri wa shughuli za kilimo chenye kuleta tija kwa taifa na tuepuke kilimo duni kwa kuwa kwa kiasi chake hakina faida.

Pia ufugaji bora kwa wanyama ambapo haitakiwi kufuga wanyama wengi katika eneo moja kwa kuwa hii hupelekea mmomonyoko wa ardhi.

Hivyo kamwe tusiharibu vyanzo vya maji.
Tupande miti na kusafisha mazingira yetu
Tunategemea utanzaji bora wa wanyamapori na misitu kwa ujumla kwa sababu maisha yetu bora hutegemea wanyamapori hao licha ya kujipatia ongezeko la fedha za kigeni pia ubora wa mazingira yetu huimarishwa zaidi.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom