KIDUNDULIMA
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 966
- 540
Leo usiku jirani yangu katoa kichapo cha nguvu kwa mwamamke wake (nyumba ndogo yake). Mwanamke kapiga mayowe kuwa jamani nisaidieni nakufa. kweli watu tukatoka mbio na tulipofika tukakuta mwanamke anavuja damu na mwanamme anamburuza mwanamke kumpeleka mahali kusiko julikana. majirani zangu walisimama pembeni kimya wakitazama tu.
Nilipofika nikauliza kulikoni. Yule mwanamme akasema nimuulize mkewe aseme nani kamlipia kodi ya nyumba wakati yeye hajampatia hiyo hela. nilipomuuliza mkewe jamaa kanibadirikia nakuanza kunitukana, mara ho naingilia mambo yasiyonihusu. Mbaya zaidi mkewe alikuwa anakataa katakata kuondoka akisema kuwa huko anakotaka kumpeleka atakwenda kumuua. Mi kuona vile nikamwambia jamaa kuwa nakwenda kumwita mjumbe. Jamaa akasema kuwa hatishiki na mjumbe na hawamfanyi lolote.
Kweli mjumbe (mjumbe mweenyewe hana hiyana maana ni baunsa na alipofika tuu alitoa mkwala mzito kwa jamaa kuwa kwa nini anasumbua watu usiku wa manane) Jamaa alinyong'onyea na kuanza kuomba msamaha. Akasema kuwa ni kiloba kimoja cha konyagi kimemfanya afikie kufanya ukatili wa namna ile. Mjumbe aliwasii jamaa na mwanamke wake warudi ndani, lakini mwanamke aligoma akalala nje mpaka asubuhi. mwanamme hasira zilipomuisha alirudi kumbembeleza mwanamke, mwanamke akakubari kurudi ndani na stori ya huko ndani hakuna anaeijua.
Ndipo ninapo uliza ni wakati gani tusiingilie ugomvi wa mme na mke na huku kukiwa na taarifa lukuki za wanawake kuuawa na kuwekwa ulemavu wa maisha.
karibuni wana JF tujadiri