Kuna watu wakipewa udaktari wa heshima wanautumia katika CV na kujitambulisha nao kila mahali kuwa wao ni ma Dr. Je hii ni sawa? Maana nasikia mara kwa mara rais wetu akiitwa Dr. kama mtu aliyesomea na kufuzu udaktari. Hivi hakuna taratibu za kudhibiti watu kupewa udaktari wa bwerere na kutamba nao mitaani? Nasikia Obama nae anao lakini hata siku moja sijasikia vyombo vya habari vikimtambulisha kama Dr. Hawa wa kwetu wanaopenda kuringia udaktari wa kupewa hakuna namna ya kuwadhibiti?