NI WAKATI GANI WAWEZA KUJIITA "NEW"

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Rafiki yangu wa siku nyingi amestaafu miaka mitatu iliyopita. Baada ya kupata kiinua mgongo chake akaamua kutafuta washauri jinsi gani atumie fedha zake katika miradi mbali mbali ili iwe endelevu na asidhalilike mjini kwa kutupiwa maneno ya shombo kwamba anaishi maisha mabovu wakati alikuwa mtumishi.
Tulimshauri ajenge au anunue nyumba kisha aifanye nyumba ya kulala wageni (maarufu Guest House). Kwa bahati mtaani kwetu kulikuwa na Guest House moja imechoka inaitwa SISIMKA GUEST HOUSE. Ninaposema imechoka namaanisha ilichoka kwelikweli maana watu wakikusikia ulipeleka mgeni wako SISIMKA au eti umelala SISIMKA, utashiba maneno ya kashfa. Wengine hata kuonekana anatokea upande wa SISIMKA walijihisi aibu.Aliinunua na kuanza kuikarabati, lakini nilichokiona kwa rafiki yangu alijali zaidi muonekano wa nje maana vyumbani aliacha vitanda, magodoro na mashuka yaleyale. Aliibadiliaha jina akaiita "NEW SISIMKA GUEST HOUSE". Aliporidhika na ukarabati alifungua biashara. Lakini kila aliyeingia hakuridhika na mabadiliko yale maana Mali za wateja ziliendelea kuibiwa kama awali na huduma zilizoonekana kuboreshwa ilidhihirika ni danganya Toto. Watumishi wake walilipwa mshahara uleule wa awali. Ndipo jamaa mmoja kidomodomo akaniambia siku moja; Hakuna kilichobadilika kwenye Guest ya rafiki yako, yaani kipya pale ni neno NEW tu".
Nimeyakumbuka maneno yake Leo kwa sababu kila nikitembea mjini naona maneno New Millenium Lodge, New Mataputapu Bar, New Chichim Hotel nk. Lakini wanaotuandikia hivi ni kweli kila kilichomo ndani pamoja na huduma ni " NEW" kweli? Au wizi wa Mali za wateja uko vilevle, chenji za wateja hamrudishi....!! Ukisema NEW tunataka kuona UPYA kweli, vinginevyo hatutaki jina NEW!! lisiloakisi UPYA.
 
Mkuu nachoelewa mm biashara ni wito kama ulivyo uwalimu ,

Nikiwa na maana moja uwe na kichwa na kipawa cha biashara si kila mtu anaweza kufanya biashara na ikastawi na kumea ,

Biashara inataka ubunifu kujituma na kujitolea ili baadae uvune natunda ya biashara husika kinyume chake utateketeza hela ...

maana kwenye biashara ni unazika hela unaimwagilia ili ije iote hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…