Ni wakati muafaka kwa Serikali kumpangia Maxence Melo majukumu makubwa ya Kitaifa kwa Maslahi mapana ya nchi yetu

Ni wakati muafaka kwa Serikali kumpangia Maxence Melo majukumu makubwa ya Kitaifa kwa Maslahi mapana ya nchi yetu

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Ndugu zangu wa JF

Naongea kwa upendo na uzalendo mkubwa kwa nchi yangu ya Tanzania

Namzunguzia Ndg Maxence Melo

Huu ni wakati muafaka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua na kumpangia Maxence Melo majukumu makubwa ya Kitaifa. Amekuwa na Utumishi uliotukuka akiwa Mtendaji Mkuu wa Jamii Forums kuanzia 2006. Kipaji chake ni kikubwa bila kusahau ubunifu wake wa hali ya juu

Amepitia na kukabiliana na changamoto mbalimbali kubwa na ndogo za amemudu kukabiliana nazo kikamilifu. Amekuwa na mchango mkubwa kwa nchi yetu kupitia jukwaa maarufu la Mtandao wa Jamii Forums. Amepoekea tuzo mbambalimbali za kimataifa kutokana na kazi zake zilizojaa Weledi mkubwa

Anafahamika, anakubalika pakubwa ndani na nje ya nchi yetu. Ni mtu jasiri na mwenye msimamo usioyumba asiyeogopa kusema na kutetea ukweli. Ni msomi mkubwa, mchapakazi, nwenye Weledi mkubwa kwenye fani yake

Ni Wakati wa kuzika tofauti zilizopo na kumpangia majukumu makubwa ya Kitaifa

Nawasilisha
 
Akina Tony Blair watakubali kweli..?
 
Marekani walimpatia Trump Urais, walimpa mamlaka hayo kwa mhula mmoja pekee. Kupata mafanikio sehemu moja haimaanisha utafanikiwa kila sehemu.
 
Miaka kadhaa iliyopita wakati tunatoka Ocean Road kutembelea wagonjwa, Max aliwahi nieleza jinsi jamaa walivyokua wanamsumbua! Nilimuelewa sana na natamani aendelee kubakia hapa hapa. He is a great Man na ana misimamo thabiti
 
You are wrong, pale watakapompa majukumu ya kiutendaji serikalini ndo utakuwa mwanzo wa hiki kitu kikubwa alichokiazisha kuporomoka. Ni vizuri hasijiingize kwenye serikali abaki hapohapo alipo.
 
Ndugu zangu wa JF

Naongea kwa upendo na uzalendo mkubwa kwa nchi yangu ya Tanzania

Namzunguzia Ndg Maxence Melo

Huu ni wakati muafaka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua na kumpangia Maxence Melo majukumu makubwa ya Kitaifa

Amekuwa na Utumishi uliotukuka akiwa Mtendaji Mkuu wa Jamii Forum kuanzia 2006

Kipaji chake ni kikubwa bila kusahau ubunifu wake wa hali ya juu

Amepitia na kukabiliana na changamoto mbalimbali kubwa na ndogo za amemudu kukabiliana nazo kikamilifu

Amekuwa na mchango mkubwa kwa nchi yetu kupitia jukwaa maarufu la Mtandao wa Jamii Forum

Amepoekea tuzo mbambalimbali za kimataifa kutokana na kazi zake zilizojaa Weledi mkubwa




Anafahamika, anakubalika pakubwa ndani na nje ya nchi yetu

Ni mtu jasiri na mwenye msimamo usioyumba asiyeogopa kusema na kutetea ukweli

Ni msomi mkubwa, mchapakazi, nwenye Weledi mkubwa kwenye fani yake

Ni Wakati wa kuzika tofauti zilizopo na kumpangia majukumu makubwa ya Kitaifa



Nawasilisha
Hawezi kuwa mtu anaweza kufuata sheria na kanuni, JF imemshinda kutokuwa na upendeleo na uoga. Uoga wake na upendeleo ulionekana wazi wakati wa uchaguzi mkuu.
 
Nyie ndo wale watu pori, watu njaa ! Ni watu mnaoamini maisha ni katika teuzi tu! Kazi ya Maxence Melo ni kubwa na pengine kubwa kuliko hata Waziri lakini kwa upeo wako mdogo unadhani Max ana njaa kama wewe!

Raia wengi wa Nchi yetu ni mbumbumbu sana ! hadi wanatia aibu!
Max anafanya na tayari amefanya kazi kubwa sana kwa Nchi hii na wala hahitaji uteuzi wowote!

Kama ni pesa akizitaka anazipiga hapahapa JamiiForum, ebu panua Kichwa chako uone kwamba hapa JamiiForum kama tuko zaidi ya watu laki nne na Maxence Melo atake kila member alipie elfu moja tu kwa mwezi basi hesabu yake itakuwa hivi:

400,000 × 1000 =400,000,000/= (Milioni mia nne kwa mwezi hiyo)! Yaani kwa akili ya Maxence Melo kila mwezi anajenga kituo kimoja cha Afya cha Wilaya cha Afya cha Magufuli.

Max ni level za akina Mark Zurgenberg wa Facebook.
Wewe maarifa yako madogo unawaza TEUZI!

Shule za Kata bomu sana!
 
Mkuu unataka atuchome kwa njagu

Akilambishwa Ajira tu hakuna siri tena jamaa atakuwa anatuchoma kwenda mbele

Wahusika futeni huu uzi kabla serikali haijaona hili wazo ikaanza mnyapia max atatuchoma balaa
 
Ni kwa vile tuu nyie ni wale mnaosemaga "forex ni utapeli" na hamna knowledge yoyote ya financial market.

Na ni kwa vile Tanzania hatuna utaratibu wa kuweka wazi utajiri wa watu wenye kampuni zenye thamani kubwa, ila kaa ukijua Max wa Jf ni kama Zuckerberg wa Fb.

Na kaa ukijua Max ana pesa ndefu kushinda matajiri wengi tuu tunaowajua, thamani ya Jf tuu inatosha kuwa tajiri namba 1 Tanzania. Kwani hii Jf akiamua kuiuza 500B hajakamata namba 1?

Mind you Max anaingia Ikulu ya White House kama nyumbani kwake tuu, wakati huohuo mama yetu pale magogoni hata kuonana na VP tuu wa USA ilishindikana.

Thread 'Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo atinga Ikulu ya Marekani (White House), awapa ujumbe vijana' Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo atinga Ikulu ya Marekani (White House), awapa ujumbe vijana
 
Read the headline carefully
" Ni wakati muafaka kwa Serikali kumpangia Maxence Melo majukumu makubwa ya Kitaifa kwa Maslahi mapana ya nchi yetu "

Kama US na kwingineko hawajafanya hivyo na sisi tusifanye ?

You just wrote a great vision. Mtu anaweza kuona Potential yake at national level kwa mapana sana ila tu changamoto kubwa ni aina ya Siasa zinazo fanywa Tanzania.
 
Simlaumu mleta mada

Msichokijua n kwamba mawazo mengi ya watanzania yameelekea huko tunaamin bila ajira au teuz serikalin basi huwezi kutoboa

...Elimu inahtajika Sana kwa vijana Kama mawazo yenyewe ndio haya ...


Vijana n taifa la leo lakn kwa mawazo haya ya mleta mada MM NAONA VIJANA N TAIFA LA JUZI ...
 
Back
Top Bottom