Ni wakati muafaka sasa Diamond aanze kuimba kwenye bar grocery za mitaani.

Ni wakati muafaka sasa Diamond aanze kuimba kwenye bar grocery za mitaani.

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Ushauri wangu kwa Diamond kua wakati ni ukuta na hakuna anaeweza kupambana nao.

Hakuna asiejua kua kwa miaka 8 iliyopita Diamond ametawala kwenye soko la muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla, hakuna.

Baada ya Diamond kupanda chati sana hapa nchini na nje ya nchi aliacha kuperform kwenye matamasha na kumbi zetu za starehe(ukiacha wasafi festival) kwa sababu kua wanalipa pesa kidogo, kuna kipindi nilisikia kua alisema Mbeya hakuna hoteli ya hadhi yake kulala. Hivyo Diamond akatusahau sisi mashabiki wake wa nyumbani tuliompandisha chati kwa vijipesa vyetu, alipofika juu akasema hvyo vijipesa havitoshi yeye kutupatia burudani.

Sasa wakati unakimbia sana, ufalme unaanza kjmomonyoka na soon utaanguka, soko kubwa la mziki wa Diamond ilikua Kenya(mziki wa Diamond unapendwa sana Kenya ila Alikiba anapemdwa Kenya), ndugu zetu wakenya wameanza figisu na asishangae akifika kule akakutana na kesi ya kukwepa kodi na kutakatisha pesa ikammaliza.

Ni wakati muafaka sasa Diamond kurudi kutuburudisha sisi mashabiki wake kwenye bar zetu kama anavyofanya mwenzake Alikiba, nyumbani ni nyumbani.

Diamond, swallow your pride, stand up like a man na uje kwenye vibanda vyetu mashabiki wako utupatie burudani.
 
Wasanii wanapojaribu kujiweka wa gharama kidogo ili waweze kuona matunda ya sanaa yao mnawasema,wakiperfom kwenye shoo za mchangani maneno pia

Lazima msanii ujue thamani yako siyo kila show tu wewe upo,na kwenye hilo Diamond amesaidia sana katika kuwaamsha wasanii wenzake wengi tu wakajua thamani yao!

Kuhusu hilo la Mbeya nadhani ni watu wenye chuki tu waliamua kumchafua tu,unaweza ukatuwekea hapa link ya kavideo labda,au ukatueleza ni wapi labda alizungumza maneno hayo!
 
Ushauri wangu wa burr kwa Diamond kua wakati ni ukuta na hakuna anaeweza kupambana nao.

Hakuna asiejua kua kwa miaka 8 iliyopita Diamond ametawala kwenye soko la muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla, hakuna.

Baada ya Diamond kupanda chati sana hapa nchini na nje ya nchi aliacha kuperform kwenye matamasha na kumbi zetu za starehe(ukiacha wasafi festival) kwa sababu kua wanalipa pesa kidogo, kuna kipindi nilisikia kua alisema Mbeya hakuna hoteli ya hadhi yake kulala. Hivyo Diamond akatusahau sisi mashabiki wake wa nyumbani tuliompandisha chati kwa vijipesa vyetu, alipofika juu akasema hvyo vijipesa havitoshi yeye kutupatia burudani.

Sasa wakati unakimbia sana, ufalme unaanza kjmomonyoka na soon utaanguka, soko kubwa la mziki wa Diamond ilikua Kenya(mziki wa Diamond unapendwa sana Kenya ila Alikiba anapemdwa Kenya), ndugu zetu wakenya wameanza figisu na asishangae akifika kule akakutana na kesi ya kukwepa kodi na kutakatisha pesa ikammaliza.

Ni wakati muafaka sasa Diamond kurudi kutuburudisha sisi mashabiki wake kwenye barr zetu kama anavyofanya mwenzake Alikiba, nyumbani ni nyumbani.

Diamond, swallow your pride, stand up like a man na uje kwenye vibanda vyetu mashabiki wako utupatie burudani.
Mbeya hakuna hotel ya kulala yeye???....mbona alikuja kyela Ngonga beach alilala tena siku mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani mwanaume mwenzio anakunyima usingizi kweli?
Mi hata sielewi imekaaje hii, mafanikio hayapo chini, yapo juu, hivyo unatakiwa uwe high ili uyafikie na sio uwe low, hutofanikiwa kamwe, Kenya ni nchi moja ndogo katika dunia. Hivyo ni wakati sasa Diamond aendelee kujitangaza kimataifa zaidi aachane na hao viburushuti wa Kenya, aendelee ku focus mziki wake na biashara zake sasa. Wa Tz. tuache wivu wa kijinga tupambane ya ela yote
 
Walichosahau ni kwamba diamond mpaka anafikia hapa alipofikia alikutana na vikwazo vingi sana akavigeuza kama daraja na fursa kwake..
Kwaiyo kadri wanavyomuwekea vikwanzo ndivyo wanavyozidi kumpaisha pasipo wao kujua..

NB:yeyote anayetaka kumuangusha diamondi asimuwekee kikwazo wala chuki bali amuunge mkono kwa kila anachofanya,ukimuwekea kikwazo imekula kwako maana jamaa tokea anazaliwa tu yeye ni kukutana na vikwazo kwa kwenda mbele
 
Mimi ni mtu wa Mbeya,hebu nioneshe kavideo Diamond platnumz a.k.a Simba a.k.a mond bin laden alisema hajaona hotel ya kulala Mbeya.
Kama hauna acha ujingaaaa.
Halafu Diamond hashuki leo wala kesho sababu Tanzania na East Africa kwa ujumla hajatokea msanii wa kuziba nafasi yake.
JAPO SIKU HIZI ANAIMBA UPUMBAVU MTUPU.
 
Anatakiwa asonge mbele zaidi na kupunguza ile hali ya watu kumuona hasi katika upande mwingine;hili tatizo la familia yake asipolituliza,linaweza kumgarimu katika kazi zake;kwa watu,mashabiki au wadau wa muziki kumchukulia yeye hasi (negative) na kupoteza mapato au hata fursa zingine.
 
Umasikini mbaya sana

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mnabishana bure kuhusu hilo.Nenda You tube andika'DIAMOND APIGWA MARUFUKU KENYA'halafu usikilize clip hiyo ya dakika 7 sekunde 1 kuhusu kilichozungumzwa na "mamlaka"za Kenya.Halafu mrudi jamvini kutusimulia kuhusu kulipa kodi anapopafomu na nyimbo anazopiga zenye " elementi" ya matusi wakidai huko kwao anakatazwa kupiga nyimbo za matusi lakini Kenya anazipiga huku zikiwa hazina maadili.

Hilo kila mtu anajua ndio..sisi tunachitaka mtuekee hiyo video au link unayomuonesha diamond akisema mbeya hakuna hoteli ya hadhi yake...watanzania chuki zitawaua aisee

Msingi wa hoja ulikuwa hoteli za Mbeya kutokuwa na hadhi ya kulala Diamond au kutotakiwa kupiga mziki Kenya?Waza hoja nje ya box acha kung'ang'ania vihoja visivyokuwa na mashiko ya evidence.Tunataka kijana awe anatuwakilisha nje ya nchi,achana na mambo ya hoteli za Mbeya kwani alikokulia ni kwenye nyumba zilizo sawa na sisi wa huku Undambani,Sumbawanga.Hakuna mwenye chuki na nguli wetu huyu bali ni kurekebishana tu.Usiwe/msiwe over-reacted baadhi ya wapendwa wenu wakipewa mawazo mbadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom